Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipotangaza kuhamia CCM, leo jioni katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kata ya Lupa, wilayani humo.
ENDELEA HAPO CHINI---------
Bryson Mwasimba kutoka Chadema akikabishi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
"Sasa Nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zanguni wakati nikiwa Chadema, Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu mnisamehe, Lakini mjue kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo. Sasa kabla sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la Chadema maana linaninajisi", alisema Bryson, akiwa jukwaani baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
"Sasa ngoja nilivulie mbali hili kwanda nibaki huru", akasema Bryson wakati akilivua gwanga lake la Chadema, huku akiwa ameshikilia mdomoni kadi yake mpya ya CCM aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto).
Baada ya kulkivua gwanda, Bryson akavaa shati la kijani la CCM.
Kisha akazungumza ya moyoni, huku akimtwisha mzigo wa Lawama Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, kwamba amekuwa akimtumbukiza kwenye madeni mbalimbali kwa kutumia huduma kisha kusepa bila kulipa. Wakati akisema hayo Nape alikuwa upande wa kulia akimtazama na kumsikiliza kwa makini sana
Ikawa nderemo na hoi hoi Bryson akabebwa na wana CCM kwa furaha
No comments:
Post a Comment