Na Karoli Vinsent
KAMPUNI ya Simu za mkononi Nchini ya Tigo imewatangazia
Neema wateja wake baada ya kuzindua promosheni kabambe iitwayo “Cheza kwa
Furaha Unaposhinda kitita”itakayowawezesha watumiaji wa huduma ya Tigo pesa
kujishindia zawadi mbalimbali za fedha taslim zenye jumla ya shilling bilioni moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,Meneja Mawasiliano wa Tigo Bw.John Wanyacha amesema
kwamba promesheni hii mpya inatokana na kampuni
hiyo kuweka kipaumbele kuwapa wateja wake sababu ya kutabasamu na fursa
ya kuweza kubadilisha maisha yao kupitia
huduma za kutuma na kupokea pesa.
“Jumla ya
shilingi milioni 150 itashindaniwa.Kutakuwa na zawadi na fedha taslim milioni10
kila mwezi kwa wateja 10 kila mmoja,fedha taslim shiling milioni mbili kila wiki
kwa wateja 20 kila mmoja na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa wateja
50 kila mmoja”alisema Wanyancha
ENDELEA HAPO CHINI--------
“Aliongeza
,shindano hili ni njia mojawapo ya kuwafurahisha wateja wetu hususan msimu huu
wa sikukuu.Tunaamini kwamba hii itakuwa kama zawadi ya kipekee krismasi hii na
tunapoanza Mwaka mpya”
Kupitia
promesheni hii ya Tigo pesa “cheza kwa furaha unashinda kitita”wateja
waliosajiliwa na huduma ya tigo pesa na
kufanya miamala ya kiasi chochote cha
fedha wataingizwa maja kwa moja kwenye
droo itakayowapa nafasi ya kushinda
zawadi xs fedha taslimu.
Vilevile Wanyancha,
alizidi kufafanua kwa kusema wateja waliosajiliwa na Tigo pesa wataweza
kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma Fedha ,kununua muda wa maongezi au
kulipa Huduma mbalimbali kupitia tigo pesa
Katika hatua
nyingine Afisa huyo wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo akaitaja miamala amabayo
haitaruhusiwa kuingia kwenye droo ya shindani hilo ni pamoja na kuangalia salio
,kubadilisha pini,kuangalia taharifa fupi ya akaunti,kubadilisha lugha na
kununua Kabaang.
Huu ni
mwendelezo wa kampuni ya tigo kuwapa raha wateja wake na kuonyesha kuwajali kwa
kuzidi kuwazawadia mapesa,promesheni hii itaisha mwezi Februari 12 Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment