TANZANIA
Bara, Kilimanjaro Stars itamenyana na Uganda, The Cranes katika Robo
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Challenge, Desemba 7, mwaka huu Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya.
Hiyo
inafuatia Zambia kuifunga Somalia mabao 4-0 katika mchezo wa pili wa
Kundi B jioni hii Uwanja wa Afraha, Nakuru, Kenya, huo ukiwa ushindi
mkubwa zaidi katika mashindano hayo hadi sasa.
Mabao ya Zambia yamefungwa na Bornwell Mwape na Festus Mbewe, kila mmoja mawili.
Katika
mchezo uliotangulia, bao pekee la Mbwana Ally Samatta kwa kichwa dakika
ya saba tu ya mchezo huo, akiunganisha krosi maridadi ya mshambuliaji
mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu liliipa Stars ushindi wa
1-0 dhidi ya Burundi.
Ikumbukwe
mara ya mwisho Stars ilipokutana na The Cranes yenye wachezaji nyota
kama Emmanuel Okwi aliyewahi kuchezea Simba na Hamisi Kiiza anayechezea
Yanga za Dar es Salaam, ilifungwa mabao 3-0 mwaka jana katika Nusu
Fainali mjini Kampala, Uganda.
No comments:
Post a Comment