KAMISHNA KOVA AKIZUNGUMZA NA WAAMDHISHI WA HABARI LEO |
Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana ya kuzuia
na kudhibiti uhalifu jijini D’Salaam hadi ngazi ya Kata. Sasa tumeamua kupeleka huduma za ulinzi
karibu zaidi na wananchi hadi ngazi za mitaa.
Wenyeviti
wa Serikali za Mitaa watashirikiana kwa karibu na wakuu wa vituo vya Polisi
ambao watawajibika kupanga askari wa vikosi mbali mbali katika kila mtaa ili
kuhakikisha kwamba mitaa yote jijini D’Salaam ina ulinzi wa kutosha. Kila mtaa utapangwa askari katika mtindo wa
wenye eneo la doria inayokidhi mahitaji ya usalama (Beat Area), Askari
watakaopangwa hapo ni pamoja na askari wa kawaida (GD), askari wa Upelelezi,
Askari wa Usalama Barabarani nk.
Askari hao watashirikiana na vikundi vya
Ulinzi Shirikishi na raia wema wa eneo hilo.
Aidha wadau mbali mbali watasaidiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja
na wafanyabiashara na wananchi kwa jumla ili kuhakikisha kwamba kila mtaa
jijini D’Salaam unakuwa huru katika suala la uhalifu.
Program hii inaenda sambamba na dhana ya Polisi
Jamii na maboresho yanayoendelea katika Jeshi la Polisi.Kila mwanamtaa ajione
kwamba anao wajibu wa kuchangia katika suala la Ulinzi na Usalama katika mtaa
wake.
No comments:
Post a Comment