WAZIRI WA KAZI NA AJIRA GAUDENSIA KABAKA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Wizara ya kazi na ajira leo imetangaza rasmi kuwa
kuna mawakala ambao wanawatafutia watu kazi ambao ni feki na wanaitia serikali
hasara ya pesa nyingi kitu ambacho wamesema ni janga kwa taifa ambapo
wamesitisha mara moja utaratibu huo ili utaratibu ufwate
Akizungumza
na wanandishi wa habari jijini dare s salaam leo waziri wa kazi na ajira mama
GAUDENSIA KABAKA amesema kumekuwa na mfumuko wa mawakala wanaojitoa kuwasaiidia
vijana kupaja ajira kwa maslai yao huku akiitaja kampuni mja maarufu Tanzania kwa
kazi hiyo ambao NI EROLINK TANZANIA ambayo imekuwa ikishutumiwa kwa kuwatesa
sana vijana wa kitanzania na kuwatumikisha pasipo haki zao za msingi kama
wafanya kazi halali
Waziri
KABAKA amesema kuwa EROLINK ni mawakala feki na hawapo kisheria na tayari
wamekwisha iingizia serikali hasara ya bilion tatu kwa miaka mitatu jambo
ambalo amesema kuwa lazima walifwatiliie kuona jinsi ya kuwaadhibu watu hao
kisheria.
“Tunawapa
mwezi mmoja mawakala hawa waje ofisini kwetu ili wasjisajili kwa mujibu wa
sheria kwani tunatambua mchango wao na tunawahitaji sana ila lazima wafanye
kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kiwanyanyasa watanzania kwa sababu
ajira inekia ngumu”alisema waziri kabaka.
JITIHADA ZA KUWATAFURA WAHUSIKA WA EROLINK KUELEZEA
TUHUMA HIZO ZINAENDELEA KAMA UNAHUSIKA TUPIGIE 0712098645
|
No comments:
Post a Comment