Tuesday, January 28, 2014

breaking newzzz---CCM YAFANYA MKUTANO MKUBWA TANDALE JIONI HII,IDDI AZANI NA MADABIDA WAFNIKA WASEMA HAKUNA CHA SERIKALI TATU HAPA NI MWENDO WA SEREKALI MBILI HADI MWISHO WA DUNIA

BURUDANI KAMA KAWA

         Chama cha mapinduzi ccm jioni hii kimefanya mkutano mkubwa jijini dar es salaam katika kata za tandalemkutano wa muendelezo wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa cham hicho  ambapo viongozi mbalimbali wa chama hicho wamehudhuria akiwemo mbunge wa kinondoni mh IDDI AZAN pamoja na mwenyekiti wa chama mkoa wa dare s salaam  hicho mh RAMADHANI MADABIDA ambapo wamezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo swala la katiba na serikali tatu.
MAMIA YA WAKAZI WA TANDALE WAKIWASILIZA VIONGOZI WAO

KARIBU UZUNGUMZE NA WANANCHI WAKO BABA

MBUNGE WA JIMBO LLA KINONDONI MH IDDI AZANIA KIWAHUTUBIA WAKAZI WA TANDALE MUDA MFUPI ULIOPITA
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la kinondoni mh IDDI AZAN amesema kuwa ccm imetekeleza mambo mengi tofauti na mambo ambayo wapinzani wamekuwa wakiyasema kuwa hayaendi na kuwabeza jambo ambalo amesema kuwa ni uongo kwani bila ccm mambo mengi hayawezi kwenda

MWENYEKITI WA CCM MKA WA DAR ES SALAM ALIKUWA MGENI RASM KATIKA MKUTANO HIO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM AMBAPO
Akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa tendele jijini leo amesema kuwa serikali mbili ni msimamo wa chama cha mapinduzi na hakuna wa kuwababaisha katika hilo kwani wana sababu nyingi za kusimamia swala hilo na wanaotaka serikali tatu wana yao mambo na ni wasaliti wan chi yao.
“hatuwezi kuwa na serikali tatu bila ya kuvunja muungano hivyo kuvunja muungano ni usaliti kwa waasisi wa nchi hii na tutakuwa hatujawatendea haki watanzania na wapenda amani wanchi hii”amesema madabida
Ameongeza kuwa mtu anayetaka mfumo wa serikali yatu haitakii mema nchi ya Tanzania na ni msaliti mkubwa nahafai katika nchi hii,kwani Tanzania imepatikana kwa taabu hivyo haiwezi kuvunjwa kirahisi kama watu wanavyofikiria na huo ndio msimamo wa chama

No comments: