MADAKTARI
VPL KUWASILISHA VYETI TFF
Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupitia klabu zao
wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8 mwaka huu.
ENDELEA--------
Wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili
kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa
wachezaji.
Pia TFF itatoa kwa madaktari hao fomu
maalumu za vipimo kwa wachezaji ambapo kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo
vyote kama ambavyo fomu imeelekeza.
Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa
kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo
hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya
wachezaji.
VPL
KUTIMUA VUMBI TANGA, BUKOBA, DAR
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
inaendelea kesho (Januari 29 mwaka huu) kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga
kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini.
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh.
5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja
wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh.
5,000.
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa
na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000
na sh. 3,000.
Azam itaumana na Rhino Rangers katika
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh.
3,000.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari na Mawasiliano
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment