Na Karoli Vinsent.
CHAMA
chaMapinduzi CCM kimemtaka Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory
Amani,kuondoka Ofisini maramoja lasivyo chama hicho kitamchukulia hatua ya
kumfukuza uwanachama.
Akitoa ufafanua
uamuzi huo Katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM, Nape Nnauye,wakati
anaongea na mwandishi wa Mtandao huu alisema haoni sababu ya Meya kukaa ofisini
hakati teyali ameshaachia ngazi.
“Mimi mwenyewe nimepigania suala hili sana hadi watu wengine
wakaanza kunichukia kuhusu uwajibikaji wangu kuhusu ufisadi wa meya
Amani,lakini leo ripoti ya mkaguzi wa Serikali imeonyesha ufisadi mkubwa sana,leo
nashangaa bado yupo ofisini. Jambo la ajabu sana, wakati tayari
alishajiuzulu na Barua yake mimi nimeiyona sasa anatafuta nini ofisini”alisema
Nnauye
Vilevile Nnauye, alisema kama akizidi kukaidi amri ya Chama
cha CCM na Viongozi wa Mkoa wa Bukoba basi chama kitamfukuza uwanachama
na Udiwani ambao anao ataukosa.
Ikumbukwe, Januari 17, mwaka huu, Amani alikubali agizo la
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya CAG kuthibitisha kuwa miradi aliyokuwa
akiitekeleza katika manispaa hiyo ilikiuka utaratibu na haikuwashirikisha
madiwani.
Mbali na Amani, wengine waliowajibishwa kwa kuvuliwa
madaraka ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamis Kaputa,
aliyekuwa amehamia Mbeya, Mhandisi wa Halmashauri, Steven Nzihirwa na Mhasibu,
Hamdun Ulomy.
No comments:
Post a Comment