Saturday, January 4, 2014

HABARI MPYA---HII NDIO SABABU YA MGOGORO WA CHADEMA,MAKUBWA YAIBUKA,KASHFA NZITO YA UFISADI YAWAANGUKIA MBOWE NA WENZAKE,SOMA MAKALA HII HAPA



Na Karoli Vinsent
   NA KAROLI VICENT

    UCHUNGUZI uliofanya na Habari24 umebaini chanzo cha Mgogoro mzito ndani ya Chama Cha Demokrasia Chadema.
   
     ,Taarifa za uhakika toka vyanzo vya kuaminika ndani ya chadema zinasema  kuwa Viongozi wakuu wa chadema  wanahofia Kuitisha baraza kuu la chadema Taifa kutokana na kutoungwa mkono na baraza hilo.
               
       Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa Mtandao huu umebaini baraza hilo linaundwa na wajumbe wafuatao
Wenyekiti wa chadema mikoa yote Tanzania,Wenyekiti wa Chadema Wilaya zote Tanzania,Viongozi wote wa Taifa.
ENDELEA HAPO CHINI-----

  Uchunguzi huu umebaini Mbunge wa kigoma Kaskazi Zitto Kabwe  ambaye alikuwa Naibu katibu mkuu wa chama hicho.kuwa na ushawishi  mkubwa ndani ya Baraza kuu la taifa la Chadema
     Taharifa hiyo inasema msingi mkuu wa Zitto Kabwe kukubalika ni kutokana na misimamo yake ya kutaka viongozi  wa mikoa na wilaya waanze kulipwa mishara ili kuongeza ufanyaji kazi katika utendaji wao ,kwani amewaaminisha wajumbe wa baraza kuu kuwa sasa chama kinapata zaidi ya Tsh.miliono 380 kwa mwezi kutokana na ruzuku kutoka serikalini,pia chama kinapata zaidi ya milioni 200 toka huko ughaibuni kwa vyama marafiki.

     Mwandishi, wa mtandao alibaini Chama cha Chadema kinapata milioni 600 kwa mwezi hivyo lazima viongozi
  viongozi wa mikoa,majimbo na wilaya zote walipwe mishahara walau kidogo kuliko mamilioni yote hayo kutumika makao makuu.
 
      Mtandao, huu umebaini kutokana ukweli huo,wajumbe wengi kutoka mikoa mbalimbali wanahamasa kubwa kufanya tukio la kihistoria litaiandikia chama hicho kikuu cha upinzani kama endapo chama hicho kitakapo kitakapoitisha baraza la mkutano mkuu na uenda wajumbe hao wakapiga kura za siri za kutokuwa na imani na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe pamoja na Katibu wa chama hicho Dk Slaa.

    Taharifa kutoka kwa makada wa juu wa chama hicho zinasema sheria ya chama hicho cha siasa kinatoa Nguvu ya Sheria kwa baraza kuu kupitia Rufaa zote za Wanachama  ambao wataona kuwa hawakufanyiwa haki na kamati kuu ,
     
    Katika hali ya Kushangaza  Mwanasheria wa Chama hicho na Pia ni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu pamoja na mwenyekiti wa chama hicho kutoona kifungu hicho cha sheria na kuendelea  kupinga Baraza kuu la Chama hicho lisifanyike,
      
    Kesi aliyofungua Zitto Kabwe Katika hoja ya msingi iliyowasilishwa na Zitto kupitia wakili wake Msando mahakamani kuu juzi, anaiomba Mahakama Kuu kuwazuia washitakiwa kwa pamoja ambao ni Kamati Kuu ya CHADEMA au chombo chochote kwa makusudi, kujadili au kuamua suala la uanachama wake.
       
       Maombi mengine ya Zitto ni kutaka apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu iliyoketi hivi karibuni na kumvua uanachama ili aweze kukata rufaa kwa Baraza la Uongozi la CHADEMA.
      
       Katika ombi la tatu, Zitto anaiomba mahakama iwazuie washitakiwa kuingilia kati wajibu na majukumu yake ikiwemo majukumu yake kama mbunge wa Kigoma Kaskazini

No comments: