KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM SULEMAN KOVA AKIONYESHA NGOZI MBLI ZA CHUI AMBAZO ZIMEKAMATWA NA POLISI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar
es salaam limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa MWAJUMA D/O HAMIS, Mkazi wa Yombo
Vituka kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni ngozi mbili za Chui,
thamani yake inakadiriwa kufikia shilingi za kitanzania millioni 11,259,500/=.
Tukio
hili lilitokea tarehe 18/01/2014 huko maeneo ya Yombo Vituka (W) Chang’ombe (M)
Temeke baada ya mtoa taarifa ambaye ni Afisa Mhifadhi Wanyama Pori mkazi wa
Ukonga kutoa taarifa kituoni hapo kuwa huko maeneo ya Yombo kuna mwananchi
anauza ngozi za chui.
Askari
walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa na walipopekua chumbani kwake
walikuta nyara hizo. Upelelezi wa shauri hilo unaendelea.
|
No comments:
Post a Comment