Mratibu
wa Promosheni za Tigo Pesa Bi. Mary Rutta (kulia) akimkabidhi mfano wa
hundi mshindi wa shilingi milioni 10 wa promosheni ya 'Shinda Kitita na
Tigo Pesa' Bi. Hilder Nyambo mkazi wa Kinondoni. Jumla ya shilingi
milioni 160 zilishindaniwa katika droo ya pili wiki iliyoisha, watano
wakijishindia milioni 5, wengine 20 milioni 2 kila mmoja na wateja 350
wakijishindia shilingi laki 2 kila mmoja
|
Mratibu wa Promosheni za Tigo Pesa Bi. Mary Rutta (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa shilingi milioni 10 wa promosheni ya 'Shinda Kitita na Tigo Pesa' Bi. Magdalena Assei mkazi wa Kigamboni. Jumla ya shilingi milioni 160 zilishindaniwa katika droo ya pili wiki iliyoisha, watano wakijishindia milioni 5, wengine ishirini milioni 2 kila mmoja na wateja 350 wakijishindia shilingi laki 2 kila mmoja |
.
Karoli Vinsent
KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Tigo leo imekabidhi zawadi za
fedha taslimu zenye thamani ya shilingi 160m/-
kwa washindi 375 wa promosheni ya ‘Cheza
Unaposhinda Kitita na Tigo Pesa’ katika hafla iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Hii ni mara ya pili kwa kipindi cha wiki moja kwa Tigo kutoa
zawadi kwa washindi wa promosheni ya Tigo Pesa. Washindi wa kwanza wapatao 275
walitangazwa na kuzawadiwa jumal ya shilingi 90m/- wakati wa sikuu ya Krismasi.
Akizungumza katika makabidhiano yaliyofanyika makao makuu ya
kampuni hiyo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, Mratibu wa Promosheni wa
Tigo Pesa Mary Rutta aliwapongeza washindi, akisema kwamba kampuni ya Tigo siku
zote inayofuraha kuweka tabasamu katika nyuso za wateja wao, hususan wakati huu
wa sikukuu ya Mwaka Mpya.
“Siku zote Tigo imekuwa ikijipanga kutimiza zaidi ya
matarajio ya wateja wetu. Na promosheni hii ina malengo ya kufanya hivyo,
kuwapa furaha wateja wetu wakati huu wa sikukuu pamoja na kuboresha maisha ya
Watanzania kupitia zawadi ya fedha taslimu,” alisema Rutta.
Mratibu huyo wa promosheni alisema kwamba washindi hao ni
kati ya maelfu wanaotarajiwa kufaidika na promosheni hii ya miezi miwili
itakayoisha katikati ya mwezi Februari 2014 ambapo jumla ya shilingi bilioni
1.12 zitatolewa na kampuni hiyo.
Kuna zawadi za fedha taslimu 10m/- kushindaniwa kila mwezi
kwa wateja 10 kila mmoja, shilingi 2m/- kila wiki kwa wateja 20 kila mmoja na
shilingi 200,000/- kila siku kwa wateja 50 kila mmoja, kwa mujibu wa mratibu
huyo wa promosheni.
“Ni kwa sababu hii tunapenda kuwahamasisha wateja wa Tigo
kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa kadri wawezavyo katika muda huu uliobaki
wa promosheni ili kuwa na nafasi nzuri ya kushinda,” alisema Rutta.
Anachohitaji kufanya mteja ili kuingia kwenye droo, alisema Rutta,
ni kutumia akaunti yake ya Tigo Pesa kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza
salio au kulipia bili mbali mbali.
No comments:
Post a Comment