Na Kiza Sungura- MAELEZO Dar es Salaam
KAMATI
ya Taifa inayohusika na mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk.
William Mgimwa imetoa ratiba ya mazishi ambapo mwili wa marehemu
utawasili siku ya jumamosi tarehe nne saa saba mchana katika uwanja wa
Mwalimu Nyerere Terminal II na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B
jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera
Uratibu na Bunge) Dk. William Lukuvi alisema kamati itakayohusika na
mapokezi ya mwili wa marehemu ni ofisi ya Waziri Mkuu itakayohusika na
ndugu, viongozi na wananchi na Kamati ndogo ya mkoa wa Iringa
inayoongozwa na mkuu wa mkoa huyo Dk. Christine Ishengoma.
Dk.
Lukuvi alisema siku hiyo ya jumamosi saa kumi na moja jioni mwili
marehemu utapelekwa katika hospitali ya Lugalo na tarehe tano siku ya
jumapili saa tano na nusu asubuhi mwili wa marehemu utapelekwa
katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za
mwisho.
Alisema
ifikapo saa nane mchana mwili wa marehemu Dk. Mgimwa utapelekwa uwanja
wa ndege wa Mwalimu Nyerere Terminal I kwa ajili ya kuelekea Mkoa wa
Iringa.
Ifikapo
saa kumi kamili alasiri mwili wa marehemu utakuwa umewasili Mkoa wa
Iringa katika uwanja wa ndege Nduli na kuagwa na viongozi na wananchi
wa mkoa huo katika ukumbi wa Siasa kilimo na baada ya hapo utapelekwa
kijijini kwake Magunga.
Waziri
Lukkuvi alimalizia kwa kusema kuwa shughuli za mazishi ya Marehemu Dk.
Mgimwa zitafanyika 6.1.2014 kuanzia majira ya saa sita mchana katika
kijiji cha Magunga mkoani Iringa na atazikwa kwa heshima zote za
Kiserikali.
|
No comments:
Post a Comment