KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA HABARI TANZANIA MCT AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Braza
la habari Tanzania MCT limetangaza kupokea jumla ya kazi 907 za waandishi wa
habari ambazo zitashindaniwa katika tuzo za waandishi wa habari zitakazofanyika
mwaka huu katika ukumbi wa mlimani city march 14
Akizungumza
na wandishi wa habari leo jijini dar es salaam katibu mtendaji wa baraza hilo
bw KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa idadi hiyo ni pungufu kidogo ya kazi
zilizopelekwa mwaka jana ambapo kazi 946 zilikusanywa.
Amesema
kuwa katika waandishi waliioongoza kupeleka kazi nyingi bado wanatoka makampuni
ya mwananchi communication kama ilivyokuwa mwaka jana,huku akisisitiza
waandishi kujifunza kushiriki katika tuzo hizo kwani zitaajengea uzoefu mkubwa.
Washindi
wa tuzo hizo watakabidhia zawadi zao katika usiku wa march 14 mwaka huu katika
ukumbi wa mlimani city ambapo mgenirasmi anatarajiwa kuwa raisi wa mahakama yay
a jumuiya ya Africa mashariki mh jaji HAROLD NSEKELA
|
No comments:
Post a Comment