ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA JAMII CCJ BW RICHARD KIYABO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Mwanzilishi wa chama cha kisiasa cha CCJ ambaye kwa sasa amekikimbia chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM leo ametoa kali ya mwaka baada ya kuitaka CCM iwape adhabu wanachama wake ambao wanamiliki kadi mbili yani ya CCJ na CCM huku akiwataja kwa majina
Bw RICHARD KIYABO ambaye ndiye aliyeanzisha chama
cha CCJ leo amejitokeza mbela ya wanahabari jijini dar es salaam na kusema kuwa
amemwandikia barua makamu mwenyekiti wa ccm mh PHILIPO MANGULA akimtaka achukue
hatua kali kwa wanachama wake ambao sio waadilifu kwa chama chake na
wamekisaliti chama chao na kwenda kuanzisha CCJ kwa lengo la kukiua CCM
“nashangaa ndani ya chama bado kuna
wanacham na viongozi waandamizi wana kadi mbili yani ya CCM na CCJ na
wameshindwa hadi sasa kuzirudisha na kuomba radhi kwa wanachama kwa usaliti huo”alisema
bw KIYABO.
MAJINA YA MICHANGO YA CCJ YA KUANDAA MAANDAMANO AMBAYO VIONGOZI WA CCM NAO WANATAJWA KUCHANGIA |
Bw KIYABO pia aliayaambatanisha majina ya
wanachama wa ccm waliowahi kushiriki katika kuchanga hela kwa ajili ya
kukisaidia chama cha CCJ kufanya maandamano ya amani nchi nzima huku orodha
hiyo akiwa na majina ya viongozi wakubwa wa CCM kama mwakyembe, samweli sitta nape,anna
kilango na wenginme wengi
No comments:
Post a Comment