MBUNGE
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ametaka wana Chadema
kuunga mkono mpango wa kumfuta uanachama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu
wao, Kabwe Zitto.
“Kuna
mlolongo wa mambo yaliyofanya Chadema ikachukua hatua kali dhidi ya
Zitto, mambo hayo yamesemwa sana na viongozi wetu; Januari 3, vikao vya
chama vitaanza mchakato wa kuhitimisha suala hilo,” alisema.
“Amekwishaandikiwa barua ya kujieleza kwa nini asifukuzwe uanachama, sasa nawaulizeni wana Chadema Iringa afukuzwe au asifukuzwe ili nikifika kwenye kikao nitoe msimamo wa Iringa?” Aliuliza na sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wakijibu “afukuzweeee….”
“Amekwishaandikiwa barua ya kujieleza kwa nini asifukuzwe uanachama, sasa nawaulizeni wana Chadema Iringa afukuzwe au asifukuzwe ili nikifika kwenye kikao nitoe msimamo wa Iringa?” Aliuliza na sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wakijibu “afukuzweeee….”
Katika
mkutano wake Desemba 31, kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,
Mchungaji Msigwa alisema Zitto amekikosea mengi chama hicho, hali
iliyowanyima uvumilivu na kuamua kumwondoa katika nafasi zake zote za
uongozi.
Alisema
pamoja na kwamba alijiunga katika chama hicho akiwa na miaka 16,
umaarufu wake kisiasa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na waasisi wa chama
hicho, aki wamo Mwenyekiti Freeman Mbowe aliyekuwa akimsaidia kifedha
wakati akisoma Chuo Kikuu (cha Dar es Salaam).
Msigwa
aliwasifu baadhi ya watendaji wa Serikali, akisema wanastahili pongezi
kwa kazi nzuri wanayofanya kuwaletea wananchi maendeleo.
“Lazima
tuwe waungwana, inapotokea kuna kazi imefanywa na watendaji, ni lazima
tuwapongeze bila kujali wanaitumikia serikali ya chama gani,” alisema.
Alitaja
watendaji hao kuwa ni Mkuu wa Mkoa, Dk Christine Ishengoma, Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Dk Leticia Warioba na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe.
Aliwapongeza viongozi hao kwa kukataa stendi mpya ya mabasi ijengwe Igumbilo, pembeni mwa Mto Ruaha Mdogo.
“Najua
kuna watu walinunua viwanja kuzunguka stendi hiyo kwa gharama kubwa; na
wameniandikia barua wakinitisha, kwamba hawataiunga mkono Chadema
endapo nitaunga mkono stendi hiyo isijengwe pembeni mwa Mto huo,”
alisema.
Alisema
watu wanaotaka alifumbie macho suala la ujenzi wa stendi hiyo karibu na
chanzo hicho cha maji ni bora waondoke Chadema kuliko kuwaunga mkono.
“Mbali
na shughuli za kilimo, maji ya Mto huo ndio chanzo kikuu cha maji
yanayotumika majumbani na wakazi wa Iringa na vitongoji vyake; ikijengwa
stendi katika eneo hilo kutakuwa na uharibifu wa chanzo hicho unaoweza
kuleta madhara kwenye maji ya Mto; sikubali, bora mtoke Chadema na kura
zenu msinipe,” alisema.
No comments:
Post a Comment