NA KAROLI VICENT/RAIA MWEMA
WAZIRI wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema amewashitaki wanasiasa
wenzake, Edward Lowassa na Rostam Aziz, kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa
vitendo vyao vya kifisadi.
ENDELEA-------
Akizungumza
naGazeti moja juzi Jumatatu, Sitta alisema tayari amewasilisha vielelezo vya
ushahidi wake ndani ya chama hicho na anachosubiri kwa sasa ni majibu ya tuhuma
zake hizo.
“Tayari
nimepeleka maelezo yangu kwenye chama kwa ajili ya kuchukua hatua. Haya mambo
ninayoyazungumza kila siku si porojo bali ni ukweli na nina vielelezo vya
kuthibitisha hayo na tayari nimevipeleka kwenye chama,” alisema Sitta,
mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.
Sitta
hakutaka kuingia undani wa tuhuma alizozitoa kwa maelezo kwamba anasubiri
kwanza chama kitoe majibu ya hoja zake.
Katika
mazungumzo yake hayo na gazeti hilo, Sitta alitamka kwamba ingawa Waziri Mkuu
aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rostam Aziz, Mbunge wa zamani wa Igunga na
mfanyabiashara tajiri, ndiyo aliowataja kwa tuhuma za ufisadi, anafahamu pia
mafisadi wengine walio ndani ya CCM lakini ameamua tu kuwataja hao kwa sasa.
Sitta
alikuwa akijibu tuhuma za Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba,
aliyezungumza na gazeti hilo juzi Jumatatu na kudai kwamba chama hicho hakina
mafisadi na kwamba wanaosema hivyo wanakivuruga chama badala ya kukijenga.
Katika
maelezo yake, Makamba alisema; “Kama akina Lowassa wangekuwa mafisadi,
wangekuwa tayari wamechukuliwa hatua na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) au vyombo vingine vya dola.
“Kama
hawajachukuliwa hatua na bado ni viongozi halali waliopitishwa na chama kwenye
nyadhifa zao, basi watu hao si mafisadi. Sitta anatakiwa awataje kwa majina
mafisadi anaowasema badala ya kulitumia neno hilo kuzungumza kijumlajumla,”
alisema.
Akizungumza
kwa utulivu, Sitta alisema kisiasa, mtu haondokewi na tuhuma za ufisadi kwa
vile tu hajakamatwa na vyombo vya dola au ushahidi dhidi ya tuhuma zake
haujapatikana.
“Kwenye siasa,
mtu kujulikana kama fisadi au si fisadi hakutokani na kutokamatwa na vyombo
husika. Ni tabia ambayo mtu unaionyesha kwa jamii ndiyo inakuwa taswira yako.
“Ndiyo maana,
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa kwa
uchafu. Hata kama hakufanya makosa, kule kutuhumiwa tu ni kubaya.
“Kwa bahati
nzuri, namfahamu vizuri Makamba. Nafahamu kwamba ni miongoni mwa watu ambao
wamekuwa wakipokea pesa kutoka kwa Lowassa na Rostam. Sasa anapokuja hadharani
na kuwatetea mimi sioni cha ajabu.
“Watu kama akina Makamba ndiyo wamelea ufisadi katika nchi
hii. Ninaposema Makamba ni mlezi wa mafisadi sisemi kwa bahati mbaya bali kwa
sababu nafahamu misaada wanayompa,” alisema Sitta.
Akizungumzia
suala la kukamatwa kwa mafisadi, Sitta alisema lina ugumu kwa sababu, kwa
tabia, mafisadi ni watu wajanja na wanaofanya mambo yao katika usiri mkubwa na
wana mahusiano na watu walio katika mfumo.
Alisema kama Tanzania haitakuwa tayari kupambana na mfumo
uliopo ambao unalea mafisadi na ufisadi, itakuwa ngumu kupambana na rushwa
ambayo alisema ndiyo adui mkuu wa nchi kwa sasa.
Hii si mara ya kwanza kwa wanasiasa kuweka hadharani tuhuma
kati yao, mara ya kwanza ilikuwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
kudai Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewahi kupewa fedha na Mbunge wa
Musoma Vijijini Nimrod Mkono ili pamoja na mambo mengine, kumhujumu aliyekuwa
mgombea wa CHADEMA Musoma Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Kutokana na tuhuma hizo, Zitto naye alikuwa mkali akisema
anatumaini Mkono pia amemwambia Lissu kwamba Mbowe naye aliwahi kuchota
mabilioni kadhaa kutoka Mkono, licha ya Mkono kutambuliwa na chama hicho kuwa
ni fisadi.
Katika majibu yake kuhusu tuhuma hizo, Mbowe ambaye
ametishia kumshitaki Zitto, alisema kuchukua fedha kutoka kwa yeyote akiwamo
Rais Jakaya Kikwete au CCM si tatizo bali tatizo ni nia iliyopo kuhusu fedha
unazochukua
No comments:
Post a Comment