Na Karoli Vinsent
WAZIRI wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewashushua Nchi washirika wa
Afrika mashariki na kusema kamwe Tanzania haiwezi kuyumbishwa na watu
wanaotaka Madaraka.
Hayo
ameyasema leo jijini dare s salaam alipokuwa anazungumza na wanahabari ,ambapo
Sitta alisema Serikali ya Tanzania haiweza kuharakisha katika kujiunga na nchi
za Afrika mashariki mpaka Wananchi wa Tanzania watakaporidhia kujiunga na umoja
huo.
“Hatuwezi kuharakisha kujiunga na umoja huu wakati
huku mambo ya msingi hatuja kubaliana nao kwasababu viongozi wa nchi hizi
wanataka kuharakisha kujiunga na umoja huu ili wapate madaraka,lakini sisi
hatuwezi tukafosi kujiunga huku mambo ya msingi ambayo yanatunayataka
hayajatimiza yanaachwa.Alisema Samueli Sitta
Vilevile Waziri Sitta alivitaja vitu vya Msingi
ambavyo Vinaifanya Tanzania kutumia busara Kabla kujiunga na umoja huo.
Kuhusu sarafu moja AMESEMA ---------
Waziri Sitta, alisema “ kuhusu sarafu Moja Tanzania
inaona ni jambo Jema ila Tanzania tupewe mda hadi kufikia Miaka kumi ili tuwe
Sarafu moja ili tuwaandae watanzania kisakrojia na hiyo sarafu
moja”alisema Sitta
KUHUSU SUAL A LA VIZA
Waziri
Sitta,alisema anashangaa sana nchi hizo yaani Kesha na Uganda pamoja na Rwanda
kufosi sana suala la kuingia nchi hizi za Afrika Mashariki bila Viza na kusema
Utaratibu huo unainyima Tanzania pesa za Utarii
“Leo nashangaa
sana wenzetu hawa wanaharakisha suala la Viza ,sisi tumewaambia Tanzania bado
katika kulikubali hili kwani hili jambo litalikosesha Taifa pesa na matokeo
yake nchi ya Tanzania kuyumba kiutalii”
“Mfano leo
mgeni akatoka huko ulaya akafikia nchini Kenya na kukata viza ya nchini Kenya
harafu akataka kuja Tanzania kwenye Mbuga zetu maana Mgeni huyo atakuja bure kutokana
na kukata viza kenya na kutokuwa na Viza na nchi itakosa mapato ya
utalii”alisema Sitta
Vievile
Samweli Sitta akalizungumzia Suala la uhalifu na akasema kwa mfumo huu wa
kutokuwa na Viza itapelekea uhalifu kuongezeka sana katika nchi hizi kutokana
watu wabaya kuingia kirahisi katika nchi hizi kutokana kutokuwa na viza
“Nataka niseme leo nchi hizi zinaharakisha sana suala hili
kwa maslai yao na sisi Tanzania tumeona suala hili litapeleka uharifu
kuongezeka sana kwa mfano Tanzania leo haipokei mtu kutoka Nchini Somalia
bila kuwasiliana na nchi zenye ubalozi wetu kama Ethiopia lakini kwa mfumo huu.
kama ziko nchi katika afrika mashariki zinaubarozi wa Somalia na zikampa kibali
basi mtu huyo ataingia kirahisi Tanzania”alisema Waziri Sitta
No comments:
Post a Comment