MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM DIDAS MASABURI AKIPATA MAELEKEZO JINSI YA KUTUMIA MASHINE HIZO ZA TIGO MATIC LEO KATIKA TAWI LA TIGO MAAKI |
Kampuni ya simu za mkononi ya tigo leo imeweka record ningine baada ya kuzindua mashine yake ya pili nchini inayojulikana kwa jina la TIGO MATIC mbayo ni mashine ya kisasa yenye uwezo wa kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wake ikiwemo kuuongeza salio,mashine ambayo itafanya kazi kwa masaa 24
Katika uzinduzi huo umehudhuriwa na meya wa jiji la dar es salaam mh DIDAS MASABURI ambapo katika hutuba yake ameipongeza sana kampuni ya tigo kwa kuwa ya kwanza kuleta mashine hizo nchini pamoja na kuanzisha huduma hiyo hapa nchini.
Ameongeza kuwa huduma zinazotolewa na makampinu ya simu hapa nchini ikiwemo huduma za kibenk,mitandao na nyingine zimeleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo nchini na kuipongeza sana tigo kwa kuwa msatari wa mbele katika huduma hizo
Hii ni mashine ya pili kwa kampuni ya tigo kuzindua hapa nchini ambapo mashine hii ipo katika tawai lake la masaki huku ya kwanza ikiwa ilizinduliw mwezi uliopita katika makao yake makuu yaliyopo kijitinyama jijini dar es salaam
HII NDIO MASHINE YA KISASA INAYOJULIKANA KAMA TIGO MATIC AMBAYO NI YA PILI KWA KAMPUNI HIYO IMEZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
MASABURI AKIKATA UTEPE KASHIRIA KUANZA RASMI KUFANYA KAZI KWA MASHINE HIYO |
No comments:
Post a Comment