NA Karoli Vinsent
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo, amekemea wanasiasa wanaojitangaza kuwania uongozi
kabla ya wakati na kuweka bayana kwamba, anashukuru kutokuwa mwanasiasa kwa
kuwa mwanasiasa mara nyingi akisema ukweli anaweza kupigwa risasi.
ENDELEA-------
Pengo alitoa kauli huku ikiwa imebaki mwaka mmoja tu
kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani, hayo yalisemwaJumamosi iliyopita jijini
Dar es Salaam alipotoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa Ibada ya
Shukrani iliyoandaliwa na Wanawake Wakatoloki Tanzania (WAWATA), siku ambayo
alionyesha wasiwasi wake kuhusu umoja na upendo katika dhamira ya wanaotaka
serikali tatu ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Napenda kulisema hili wazi kwamba si kwa sababu mimi ni
mwanasiasa... nilishawaeleza tangu zamani siasa na mimi tusingeenda pamoja.
Wangekuwa wameshanipiga risasi zamani maana yake mwanasiasa ukisema ukweli
huwezi kudumu,” alisema Pengo ambaye alionekana kuzungumza kwa hisia na
uchungu.
Alisema ni hatari kwa mustakabali wa taifa kwa kila
mwanachama katika chama chochote kile kuanza kutamka kabla ya chama hakijatamka
kuhusu nafasi za kugombea uongozi wa serikali kupitia chama husika.
Kauli hiyo ya Pengo imekuja siku chache baada ya Waziri mkuu
aliyejiuzuru na pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kuonyesha nia
iliyojificha, Januari Mosi, mwaka huu nyumbani kwake kwamba anaweza kuwania
nafasi ya juu ya uongozi nchini.
Lowassa alikuwa Waziri Mkuu kabla ya kulazimika kujiuzulu
kwa shinikizo la Bunge kutokana na kuhusishwa katika kashfa ya zabuni ya umeme
wa dharura, iliyotolewa kinyemela kwa Kampuni ya Richmond Development LLC.
“Tuombee vyama vyetu vya siasa umoja na upendano, walau
ndani ya vyama kama sio chama kwa chama.. hiyo (chama kwa chama) labda
inaweza kuwa baadaye lakini ndani ya vyama kuwe na umoja na upendano. Watu
katika chama kimoja wangoje chama kinasema nini na kinateua nani wawe wagombea
wa uongozi wa taifa letu,” alisema Pengo.
Akizungumzia kuhusu serikali tatu, alisema kwa sasa
mazungumzo na dhamira ya wanaotaka serikali tatu hayatokani na nia njema na
upendo bali yanatokana na tofauti na manung’uniko kutoka pande mbili za
Muungano, hali inayoashiria kutokuwapo nia njema..
umefika mahala, kiongozi wa kidini anatamka kwenye nyumba ya
ibada;
“ Msiwachague wale wenye kutoa kofia na fulana”. Mwingine
anatamka; “ Msiwachague watakaotuletea vita.”
Katika mifano hiyo miwili ya kauli ni dhahiri, kuwa bila
kutaja ni akina nani wenye kutoa kofia na fulana waumini wameshawajua ni
akina nani. Na bila kuwataja hao ‘ watakaotuletea vita’ waumini wameshawajua ni
akina nani. Hayo mawili hayawezekani yakawa ni mafumbo magumu kwa waumini
kutoka kwa viongozi wa dini.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na Mwandishi
wa mtandao wanasema kauli aliyoisema Askofu Pengo ni ya ukweli mtupu kutokana
na hari ya vita ya kusaka urais mwaka 2015 ikiwa imshika kasi.
Wachambuzi hao ni John Jambele ambaye kwa upande wake
alisema “kitendo cha viongozi wetu kupita makanisani au misikitini na
kuanza kutoa fedha ni sawa kabisa ila tuatashangaa viongozi hawa tena baadaye
waibuke na kuanza kugombea urais tutashangaa sana kwani hata mwalimu Nyerere
alisema ukiona mtu yeyote anatumia nguvu na kumwaga pesa ila hapate Urais uje
hatufai hata kidogo”alisema Jambele
Duru za kisiasa zinasema Mvutano wa wasaka Urais ndani chama
cha Mapinduzi CCM uwenda kikaingia kwenye mgorogoro mzito kutokana na baadhi ya
wanachama kuutaka urais kwa udi na uvumba huku wengine wakitumia mamilioni ya
pesa ili wapate urais.
No comments:
Post a Comment