Kamati Kuu CHADEMA leo kimewapendekeza Prof Abdallah Safari, Mabere Marando,Nasra Juma Baruan na Method Kimomogolo ili wateuliwe na Rais Bunge la Katiba.
Professor Abdallah Safari ni mwanasheria nguli
wa chama hicho na pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.Huku
Method Kimomogolo ni mwanasheria maarufu wa Chama hicho ambaye ameongoza
kesi nyingi zilizokwishafunguliwa dhidi ya Chadema na viongozi wake.
Wasifu wa Mabere Marando kila mtu anaujua kwani ni nguli aliyeongoza
Mageuzi Tanzania tokea kabla ya mfumo wa vyama vingi.Kwa sasa ni mjumbe
wa Kamati Kuu Chadema na ni mmoja wa wanasheria wake huku akiwa pia
Makamu Mkiti wa Chadema Kanda ya Pwani.
Rais anatarajiwa kuteua majina mawili tu kutoka Chadema na kwa mujibu wa sheria ni sharti katika wateuliwa hao mmoja atoke Zanzibar na pia lazima mmoja awe mwanamke.
Rais anatarajiwa kuteua majina mawili tu kutoka Chadema na kwa mujibu wa sheria ni sharti katika wateuliwa hao mmoja atoke Zanzibar na pia lazima mmoja awe mwanamke.
No comments:
Post a Comment