Wizara
ya maliasili na utalii tanzania kupitia idara ya wanyama pori tanzania
imewasimamisha kazi watumishi wake 21 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya
hujuma juu ya wizara hiyo
akizungumza
na wanahabari leo jijini dar es salaam naibu waziri wa wizara hiy mh
LAZARO NYALANDO amesema kuwa katika watumishi waliosimamishwa 11
wanatoka kikosi dhidi ya ujangili arusha,4 pori la akiba rukwa,1 kutoka
pori la akiba seluu,3 pori la akiba maswa,na 1 kutoka pori la akiba
lukwika-lumesule-msanjeshi.
amesema
kuwa makosa makubwa yaliiyofanywa na watu hao kuw ni vitendo vya rushwa
katika mapori hayo pamoja na kuwasaidia majangili katika kufanya uhalifu
wao huo,ambapo ameeleza kusikitishwa sana na vitendo hivyo
Aidha
jana jeshi la polisi kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii
lilimkamata askari wa wanyama pori mmoja bw AGOSTINO LORI mkoani singida
akiwa na bunduki mbili na ndege aina ya heroe au flamingo 12 uani mwa
nyumba yake kinyume na sheria .
Naibu waziri amesema kuwa
mtu huyo miongoni mwa maaskari wa wanyamapori ambao wanashiriki katika
vitendo vya hujuma,rushwa,na ujangili dhidi ya wanyama porihuku akiwa
ameaminiwa na nchi yake kama askari wa wanyama pori.amesema kuwa kitendo
hiko kinatia aibu sana nchi na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa mara
moja
|
No comments:
Post a Comment