MKURUGENZI WA OGANAIZESHEN NA MAFUNZO WA CHADEMA AKIONYESHA BARUA YA TUIME YA UCHAGUZI YA KUTAMNGAZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KALENGA WAKATI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Na Karoli Vinsent
SIKU chache
kupita baada ya Rais Kikwete kumteua mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest
Mangu,Chama cha Demokrasia na Maendereo CHADEMA kimeanza kukosa imani naye.
Hayo, yamegundulika
leo wakati wa mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Chama
hicho jijini Dar es Salaam,ambapo Mkuregenzi wa Mafunzo na organaizesheni wa
chama hicho Bensoni Singo Kagaila alisema Jeshi la Polisi nchini linashirikiana
na Chama cha Mapinduzi CCM katika kukihujumu chama hicho katika mikutano yake
inayoenderea.
ENDELEA=-----------
“Nasikitika
sana fujo zote zinazotokea katika mikutano yetu ya kampeni hizi za
uchaguzi wa madiwani wa kata kumi na sita,zinasababishwa na jeshi la
polisi nchini kushirikina na chama cha mapinduzi, kwani wanachama wetu
wanapigwa wanakatwa mapanga na watu wa Greengard huku polisi wakiwa kimya na
kutochukua hatua yeyote”alisema Kagaila
Kagaila,alishangaa
kitendo cha Jeshi la polisi kuwakamata vijana wa Chadema wanaopigwa na Vijana
wa Greengard wa CCM na kuwaacha wale wanafanya Vitendo hivyo.
“Leo jeshi la
Polisi limekuwa ni la CCM na linatumiwa na chama hicho ,inasikitisha sana pale
Mkoani Iringa kijana wetu wa Chadema Kavunjwa Taya lakini waliomvunja taya
wameachwa anakuja kukamatwa aliyevunjwa taya huku watu wa CCM Waliofanya unyama
huo wameachwa jamani huu ni uonevu tunaofanyiwa na Jeshi la polisi
kushirikina na CCM“alizidi kuongeza Mkurugenzi huyo.
Kuhusu fujo za Iringa
Mkurugenzi
huyo alisema kuhusu kitendo cha Jeshi la polisi mkoani Iringa kumkamata Mbunge
wa Iringa mjini Piter Misigwa na kumweka ndani kwa mda wa siku moja ni
uonevu.
“Haingii akilini kweli mbunge huyu alikuwa anahutubia watu
jukwaani,leo jeshi la polisi liseme yeye ndie aliyempiga kijana wa CCM,huu ni
uongo kwani mbunge huyo akushuka kwenda kumpiga kijana huyu na wala kijana na
akupigwa kabisa na mtu yeyote wa chama chetu”
Kwa mujibu wa
Kagaila alisema mbunge huyo ameachiwa leo hii kwa dhamana,
Chadema
ambacho ni Chama Kikuu cha upinzani nchini,kimemtaka msajiri mpya wa vyama vya
kisiasa Nchini kupiga marufuku na pia kuwaonya wanachama wa chama cha Mapinduzi
kwa vitendo vyao vya kuingiria kwenye mikutano yao kwani ni kinyume na sheria
ya uchaguzi.
Katika hatua
nyingine Chama hicho kimetangaza nafasi kwa mtu yeyote anayetaka kugombea
nafasi ya Ubunge wa jimbo la Kalenga uliochwa wazi baada ya kifo cha
aliyekuwa mbunge wake.Dkt William Mgimwa kuomba nafasi hiyo kupitia kwenye
mtando wa chama hicho au kuandika Sifa au cv na kuzipeleka chadema makao makuu
jijini Dar es Salaam au kwenye ofisi za chama hicho mkoani iringa.
Vilevile
chama hicho kimesema mda wa kuomba nafasi hiyo ni tarehe 9 mwezi huu.na
tarehe 12 kamati kuu ya Chadema itakutana 12 mwezi huu kwa ajili ya
kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea wa ubunge wa CHADEMA jimbo la
Kalenga.
Kwa mujibu wa
Ratiba ya uchaguzi huo ulitolewa na Tume ya uchaguzi Nchini NEC,kampeni
zitazinduliwa februali 19 mwaka huu .
No comments:
Post a Comment