MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), FreemanMbowe amemjibu Rais
Jakaya Kikwete kwamba asiingize utani katika masuala mazito ya taifa
Mbowe
alisema Katiba ya Tanzania, itaamuriwa na wananchi wenyewe na si Chama Cha
Mapinduzi (CM) ambacho kimekuwa na mkakati mkali wa kutaka kuua maoni ya
wananchi.Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Kikwete
kudai amesikia kiongozi huyo wa upinzani akitangaza kutumia nguvu kupata Katiba
mpya.
ENDELEA HAPO-------
Rais
Kikwete alitoa kauli hiyo juzi kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, wakati
akihutubia sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa CCM. Alisema amesikitishwa na kauli
hiyo na kuwataka Watanzania kutobabaishwa.
Kikwete
alisema Katiba mpya itapatikana kwa hoja za kila upande kulingana na
mapendekezo yake.
Akizungumza
na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mbowe alisema Rais Kikwete hapaswi kuchukulia
utani katika mambo mazito ya taifa.
“Namuomba
Rais Kikwete asichukulie utani mambo ya taifa suala la Katiba mpya. Anapaswa
kuzungumza mambo ya msingi ambayo yanaleta tija.
“Siku
zote Katiba ya nchi inapatikana kwa dhamira nzuri lakini tumebaini wenzetu hawa
CCM hawaheshimu hoja za wananchi.
“Hebu
tujiulize jinsi Jaji Joseph Warioba alivyotumia fedha nyingi kukusanya maoni ya
Watanzania, leo CCM hao hao wanayakataa tuwaeleweje?” alihoji Mbowe.
Alisema
Jaji Warioba ametoa hoja za msingi lakini kwa sababu ya uoga wa CCM wanataka
kupindisha ukweli wa mambo.
“Mzee
wa watu huyu amezunguka taifa zima kwa fedha za walipa kodi wa nchi hii, sasa
wanataka watumie wabunge wao kukwamisha mchakato huu,”alisema Mbowe.
Alisema
kama utawala wa Rais Kikwete utashindwa kuleta Katiba mpya ambayo inakidhi
matakwa ya Watanzania, wao wataendelea kudai utawala mpya utakapoingia
madarakani uwe ni wa Chadema au CCM.
“Nawahakikisha
Watanzania, ikija Katiba mbaya tutaendelea kuidai kwa nguvu zote iwe CCM
imeingia madarakani au sisi, Kikwete awe madarakani au asiwepo hatulali kamwe.
“Katiba
ni maridhiano ambayo yanabeba maoni ya Watanzania sasa kwa nini CCM hawataki
kuyafuata?” alihoji Mbowe.
Alisema
CCM haina hatimiliki ya Katiba mpya na kwamba wakati wa kufanya uamuzi mgumu wa
kupindisha maoni ya Watanzania umefika.
“Hawa
watu hawana hatimiliki ya Katiba mpya, kwa nini wanajawa uoga kiasi hiki?
Wanaogopa serikali tatu, nakwambia sitaki utani kwenye ya msingi,”alisema
Mbowe.
NJE
YA BUNGE
Mbowe
alisema atahakikisha wanajadiliana vya kutosha ndani ya Bunge kuona haki
inatendeka.
“Tutabishana
kwa kila namna ndani ya Bunge,wakituzidi kete kwa rafu zao bungeni tutarudi kwa
wananchi kuwashitaki maana hawa ndiyo walengwa… hatutaki kufika huko kama kila
mtu ataweka busara zake chini.
“Dhamira
ya CCM ndiyo inatufanya tutoe kauli hizi lakini nakwambia hapa hakuna mcheza
ngumi… hoja ndiyo jambo la msingi tu,tutatumia maandamano nchi nzima maana haya
ni haki ya msingi ya kila mtu,”alisema Mbowe.
Chanzo
- Mtanzania
No comments:
Post a Comment