Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam TV na kuamua
kutoa pesa waliyolipwa kukilipa kituo kimoja nchini ambacho ndicho kilichopewa
kandarasi kwa malipo licha ya kutokidhi vigezo vya watu wa Egypt ambao walitaka
angala 8 Camera OB na Azam TV iliwapa 10 Camera OB with HD Feed
Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu wateja wetu
kuwa Azam TV ilikuwa tayari kuwapa Yanga na Agent ushirikiano wote ili pesa yote
waliyopewa na Watu wa Misri iingie klabuni lakini wao wameamua kuitumia kulipia
production iliyo sub-standard ili mradi tuu kuinyima fursa Azam TV
Pamoja na haya yote Azam TV inaitakia kila la kheri
klabu ya Yanga kwenye mchezo wake wa leo, na inaamini matatizo hayapo kati ya
Azam na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja mwenye nguvu ndani ya Yanga
No comments:
Post a Comment