Friday, February 28, 2014

JAMANI JAMANI MTOTO HUYU ANAITAJI MSAADA WENU WATANZANIA,INATISHA SANA,ONYESHA UPENDO KWA KUMSAIDIA.samahani kwa picha ila ndo ukweli

Mtoto Adolotea Njavike (1.4) ambaye kichwa na kiwiliwili vimeungana baada ya kupata ajali ya moto akiwa na mama yake mzazi.
Mama mkubwa wa mtoto huyo, Salome Kiegu (35) mkazi wa mtaa wa Maendeleo Iyunga jijini Mbeya anasema mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo mtoto huyo aliungua vibaya.
Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu akiwa amempakata mtoto huyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo.
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na kichwa na kiwiliwili kuungana baada ya kupata ajali ya moto akiwa na mama yake mzazi.
Akizungumza kwa masikitiko, mama mkubwa wa mtoto huyo, Salome Kiegu (35) mkazi wa mtaa wa Maendeleo Iyunga jijini Mbeya anasema mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha walipoangukia kwenye moto ambapo mtoto huyo aliungua vibaya.
Anasema tukio hilo lilitokea Agosti mwaka jana lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida wakati wa kula na kushindwa kufurahi na wenzake.

Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo wataalamu walimwambia atafute shilingi milioni moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.

Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki mtoto kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.

Aidha kutokana na maelezo hayo, Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanikisha matibabu ya mtoto wake.

Amesema anahitaji zaidi ya shilingi milioni mbili ili ziweze kumsaidia kusafiri, kugharamia matibabu pamoja na huduma nyingine wakati akisubiri matibabu ya mwanaye.

Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mama huyo kupitia simu yake ya mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga, mtaa wa Maendeleo jijini Mbeya.

No comments: