SERIKALI
kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekunjua makucha yake kwa
kutangaza kuvifuta vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) .
Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es
Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa
kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa
kusajiliwa.
Alivitaja
vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism
College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa
Institute of Business Management na Aspiration Training Center, vyote
vya Dar es Salaam.
Vingine ni Dar es Salaam School of Hair
Design, Media and Values Training Institute na Information Technology
Training Center vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro
School of Medical Sciences cha Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo.
Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo
urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa
mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa yanayotokana na wanafunzi kukosea
kujaza fomu za mikopo
No comments:
Post a Comment