Naibu waziri wa fedha ambaye ni mbunge wa bunge maalum la katiba mh MWIGULU NCHEMBA muda huu nusura alivunje bunge hilo kwa kauli zake ambazo zimmewajaza hasira na jazba wabunge wengi wa bunge hilo la katiba baada ya kuwatuhumu wabunge wenzake mh FREMAN MBOWE na MH JUSA kuwa wanataka kuleta ushoga hapa nchini ndio maana wanataka kura ya siri ili wapitishe ushoga kirahisi.
Kauli hiyo imemfanya mwenyekiti wa CUF pr IBRAHIMU LIPUMBA alipoamua kuomba muongozo kuhusu kauli hizo ambazo zimelizalilisha bunge na kuwazalilisha wabunge wote wanaounga mkono kura ya siri kuwa wanautaka ushoga nchini.
Baada ya muongozo wa lipumba makamu mwenyekiti wa bunge maalum la katiba amemtaka nchemba kuomba radhi mara moja hku wabunge wengi wakizomea kwa sauti kubwa jambo ambalo limefanya bunge kuwa la fujoo muda huu.
Tayari NCHEMBA amewaomba radhi watanzania na bunge linaendelea
No comments:
Post a Comment