Waziri mwakyembe akiwasili eneo hilo wakati wa ziara |
Na Karoli Vinsent
WAZIRI wa Uchukuzi Dokta Harrisoni
Mwakyembe leo amedondosha chozi baada ya kushuhudia hujuma iliyokuwa inafaywa
na mawakala wa Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea huduma zao zikisimama na
kuwaleta usumbufu watumiaji wa Bandari hiyo.
Hayo yaligundulika leo wakati Waziri
wa Uchukuzi Dokta harisoni Mwakyembe alipofanya Ziara ya kustukiza kwenye vituo
vya mawakala hao na kushuhudia usumbufu unaotokana na Uzembe kutoka kwa
mawakala hao.
“Nimepigiwa simu sana na wananchi
juu ya hawa mawakala wa Neah Investiment agency kuwa ni wasumbufu sana,na leo
nimekuja kushuhudia huo usumbufu kwahiyo nawaomba muwe watulivu na kunipa
ushirikiano”alisema Mwakyembe
Ndipo,Mwakyembe aliingia kwenye
Ofisi za Neah Invement agency zilizoko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam
na kushuhudia umati wa watu wakiwa hawajapata huduma yeyote kutoka kwa
kampuni hiyo huku wakisema wamefika hapo zaidi ya wiki mbili
“Hafadhari mkombozi wetu mwakyembe
umefika uje kushuhudia unyama huu tunaofanyiwa na kampuni hizi maana tumekaa
hapa wiki ya pili hiii na hatujapewa huduma yeyote badala yake tunapigwa
karenda huku mgari yetu yanakwama tu pasipo sababu”alisema mmoja ya wananchi
Baada ya kusikia kelele hizo kutoka
kwa Wananchi ndipo waziri huyo akataka kujua nini tatizo na kuwaita Viongozi wa
Kampuni hiyo na kushuhudia Urasimu mkubwa katika kuwahudumia wananchi.
“Nakuomba Meneja utuambie nini
Tatizo linalopelekea msongamano wa watu wengi hivi?
Ndipo Meneja wa kampuni hiyo
anayejulikana kwa Jina moja Muhamed akasema tatizo la msongamano wa watu
katika ofisi hiyo ni kutokana na tatizo na mtandao katika kumpyuta.
Ndipo Waziri Mwakyembe akagundua
tatizo linalopelekea foleni na adha kwa wananchi ni ukiritimba kutoka kwa
mameneja wa Kampuni hiyo kwa kushindwa kuweka benki katika ofisi hiyo
iliisiwape tabu katika kulipa fedha kwenda tra.
“Nakupa siku tatu wewe meneja
lasivyo nafunga hii ofisi yenu yaani kwaanzia leo alhamini mpaka Jumatatu kama
hamtoweka Benki humu ndani basi nitawafungia na msiendelee na Kazi na haya majengo
mliotumia pesa nyingi mfugie hata kuku”alisema Mwakyembe.
Katika hatua nyingine Waziri huyo
akashangaa jinsi wafanyakazi wa Kampuni hizo za uwakala kushindwa kufanya kazi
kwa kisingizio cha mtandao kuwa na kuwaacha Wananchi wakiteseka
No comments:
Post a Comment