Mjumbe wa jukwaa la katiba tanzania bw izrael ilunde akizungumza katika kutano huo na wanahabari juu ya uamuzi wa jukwaa la katiba kuhusu bunge la katiba tanzania |
Jukwaa la katiba Tanzania JUKATA
leo limetangaza nia yake ya kutaka kuwashawishi wananchi kuandamana hadi mjini Dodoma
kulifunga bunge la katiba endepo kama hawataridhika na bunge hilo na kama
watagundua kuwa wabunge hao hawana nia ya dhati ya kuwapatia katiba bora
wananchi.
Hayo yamesemwa leo muda huu jijini dar
es salaam na kaimu mwenyekiti wa jukwaa hilo bw HEBRON MWAKAGENDA wakati akizungumza na vyombo
mbalombalo vya habari kuhusu mwenendo wa bunge hilo maalum la katiba
linaloendelea mjini Dodoma.
Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania bw HEBRON MWAKAGENDA akizungumza na wananchi muda mfupi uliopita kuhusu bunge la katiba |
MWAKAGENDA anasema kuwa jukwaa
la katiba linaendelea kutathmini kile kinachoendelea bungeni na kama
wakijiridhisha kuwa kinachoendelea hakielekei kuwapatia watanzania katiba mpya
bali ni upotevu wa muda na rasimali za taifa basi JUKATA itatumia ibara ya nane
ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwaongoza wananchi kulifunga
bunge maalum la katiba na kuanza harakati za kuitafuta katiba mpya kwa utaratibu wenye
mantiki na tija kwa taifa.
Aidha jukwaa la katiba Tanzania limeipinga
vikali hotuba iliyotolewa na raisi wa Tanzania dk JAKAYA KIKWETE wakati
akifungua bunge hilo ambapo wamesema kuwa
hotuba ile ilifaa sana kutolewa na mwenyekiti wa chama cha siasa kwenye
mkutano wa chama husika na sio katika bunge kama lile.
Bw MWAKAGENDA anasema kuwa jukwaa
la katiba linapenda kuwataarifu watanzania wote kwa ujumla kuwa katiba
inayotengenezwa sio ya chama chochote cha siasa bali ni y watanzania wote hivyo
ni kosa kwa chama cha siasa kuuteka mchakato huo kama wao ndo wanatengeneza
katiba yao ambapo anasema kitendo cha wanasiasa kuwa na sauti kubwa katika
bunge la katiba kimeufanya mchakato wote kutekwa na kuonekana kama mchakato wa
kisiasa.
Mchakato
wa bunge la katiba unaendelea huku kukiwa na mabishano maengi ambayo watanzania
wengi wamekuwa wakishindwa kuelewa ni ya nini hadi kufikia matumizi ya matusi
na vijembe kutawala katika bunge hilo
No comments:
Post a Comment