waziri wa maliasili na utalii lazaro nyalandu alipokutana na mwandishi wa daily mail MARTIN FLETCHER nchini uingereza miezi michache iliyopita |
Na Karoli Vinsent
KILE kinachotafsiriwa ni njama ya Serikali ya Tanzania,
kujisafisha baada ya kuumbuliwa kwenye medani za kimataifa na Mwandishi wa Gazeti
la Sunday Mail la Nchini uingereza Martini Fletcher kuhusu vitendo vya
Ujangili, hivi leo Mwandishi huyo ameitwa kwenye ikulu ya Jakaya Kikwete,
Taarifa ambazo amezipata mwandishi wa Mtandao huu zinasema
Serikali ya Tanzania kwa kupitia Wizara ya Maliasili na utalii,katika kile
kinachoitwa ni kutaka kujikosha,imemwalika Mwandishi huyo wa Habari wa gazeti la
Sunday Mail,ambaye hivi karibuni aliandika makala iliyowachefua viongozi akiwemo
Rais Jakaya kikwete.
Chanzo,hicho kinasema kuwa Mwandishi huyo alialikwa na
Waziri wa Maliasili na Utalii.Lazaro Nyalandu, taarifa hiyo ilizidi kufafanua
kuwa mwandishi huyo aliwasili Jumapili na kufikia kwenye Hoteli ya kimataifa ya Serena,
Mwandishi huyo aliyewaudhi viongozi wengi wa Tanzania
wasiotaka kuambiwa ukweli,amepangiwa kuzuru kwenye pori la akiba Selous na
Hifadhi ya Serengeti.
Kwa mujibu wa Chanzo chetu zinazisema mwandishi huyo
anatarajiwa kukutana na Rais kikwete,lakini hadi sasa haijawekwa wazi ,lakini
yamekuwa mapendekezo ya kuhakikisha anakutana na rais kikwete,
Kuletwa kwa Feltcher kunaelezwa na Baadhi ya watu ni ufujaji
Fedha za umma,kwa vile haitarajiwi mwandishi huyo mahiri andike makala ya
kukanusha kile alichokiandika.
Makala ya
Fltecher kwenye Gazeti hilo la Uingereza,yaliwakasirisha
viongozi wa Tanzania hasa kutokana na ujio wake kulenga muda ambao
viongozi wa mataifa zaidi ya 50 walikuwa wamealikwa kwenye mkutano maalum
ulioitishwa na mwana wa Mfalme wa Uingereza,Prince Charles,mjini London.
Ikumbukwe Makala ya Fletcher yalichapishwa Februali 8 mwaka
huu na kuchapishwa kwenye Gazeti la Sunday Mail ambapo katika makala hiyo ilimtuhumu
Rais kikwete kwa kushindwa kuwachukulia hatua vinara wa vitendo vya ujangili
Vilevile, Makala hiyo ikizidi kumtuhumu Kikwete kwa
kumdharau aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii Barozi Khamisi Kagasheki
alipokuwa anamletea Orodha ya vinara wa vitendo vya ujangili.
Kwa upande mwengine Mwandishi huyo alisema pesa zinazotoka
na vitendo vya ujangili zinakwenda kukijenga chama cha mapinduzi CCM,
Baada,ya makala hiyo kuchapishwa ndipo Waziri wa Maliasili
na Utalii Lazaro Nyalandu akaibuka na kumpinga mwandishi huyo na kusema
serikali ya Rais jakaya Kikwete imefanya kazi kubwa ya kutokomeza vitendo vya
Ujangili nchini.
Katika hali ya kushangaza baada ya Waziri Nyalandu,kukanusha
taarifa hizo,Waziri kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Peter Msigwa
akaibuka na kusema mwandishi huyo yuko sahihi katika makala yake kwani serikali
ya Rais Kikwete inawalinda watu wanaohusika na vitendo vya ujangili nchini.
Kauli ya Msigwa ilikwenda kinyume na Rais kikwete wakati
anahojiwa kwenye kituo cha Televishini cha CNN,aliutangazia ulimwengu kuwa
anamajina 40 ya majangili hatari nchni na kiongozi wao ambaye yuko mjini
Arusha.
Kauli za aina hiyo zilizidi kumpa umaharufu mwandishi
Fletcher na kuthibitisha kile alichokisema kwenye makala yake,serikali ya
Tanzania haionyeshi utashi katika kupambana na Majangili licha ya kuwatambua.
No comments:
Post a Comment