Tigo Tanzania leo imetoa tuzo za simu
za kisasa kwa wateja wake kumi bora walioshiriki
katika utoaji maoni,ushauri kwa kampuni hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ya
Facebook na Twitter mwaka 2013.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi
kwa washindi hao jijini Dar es Salaam, Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii Tigo,
GeorgeKatoto,amesema tuzo hizi ni kwa
ajili ya kuwa tambua na kuwashukuru wateja hao kumi kwa ushiriki wao katika utoaji
maoni kwa kampuni,marafiki na jamaa zao kupitia mitandao ya Facebook na Twitter
yakampuniya Tigo mwaka uliopita.
“Kwasasa tunawafuasi zaidi ya 332,000
katika Facebook nazaidi ya wafuatiliaji 14,700 katika Twitter. Idadi hii ninzuri
nailiyotupa msukumo wa kutoa shukrani zetu kwa wafuasi wetu na wafuatiliaji wa mitandao
yetu ya kijamii. Michango yao imekuwa chachu katika kutuletea ufanisi mkubwa mwaka
wa 2013,” alisema.
Kutokana na maelezo ya Katoto,
washindi saba bora walioweza kuzawadiwa simu aina ya Huawei – Y300 pamoja na
modem yenye kifurushi cha mwezi mzima niFaudhu Abbas Kiobya, Davidy DaudLuoga, Robiascos
Jemedali, Mohamed Lukuvi, HamimuHalfan, Ibrahim JumanaAlly Ibrahim.
Watatu wengine walioshindani Pascal Chacha,Daudi
Daudna Badman Msolidia mbaonao waliweza kuzawadiwa modem yenye kifurushi cha
mwezimzima.Washindi wote pia walitunukiwa vyeti vya shukurani kutoka kampuni ya
simuya Tigo.
“Kurasaza Facebook na Twitter za Tigo zimekuwa ni jukwaa ambazo zimefanikiwa
kuwavutia maelfu ya wateja kwenye mitandao kutokana na kuwa na vitu vyenye ubunifu
na kufurahisha.
Nafurahia sana kushirikina marafiki
nawenzangu wengine kupitia ukurasa zao.
Napenda kuwa shukuru sana kwa kunitambua kwanamnahii ya kipekee,”
alisema Kiobya, mshindiwa kwanza.
Katoto aliendelea kusema kwamba vigezo
vilivyotumika katika kuwa chagua washindi hao ni kuwa washiriki bora katika kuanzishamada,
kuchangiamada, kusambaza na kupiga ‘like’, pamoja na kushiriki katika ‘Live
Chat’ zakurasa za Facebook na Twitter za kampuni hiyo.
|
No comments:
Post a Comment