AFISA MRADI WA RACHEL NDAUKA AKIZUNGUMZA |
NA EXAUD MTEI
Wafanyabiashara wa kariakoo
mwezi huu watapata nafasi ya kuonyesha biashara zao katika viwanja wa coco
beach jijini dar es salaam kwa mara ya kwanza Tanzania ktika maonyesho ya
kibiashara yanayojulikana kama KARIAKOO@COCO BEACH yaliyoandaliwa na HAZINA
CAPITAL maonyesho ambayo yatafanyika march 29 na 30 na baadae kuendelea kila weakiend ya mwisho wa mwezi.
Akizungumza na wanahabari leo jijini
dar es salaam meneja mradi wa HAZINA CAPITAL RACHEL NDAUKA amesema kuwa
maonyesho hayo ambayo yatashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 25 hadi 50 yanalenga kuwapa wafanyabiashara wa kariakoo
kuuza bidhaa zao katika maonyesho hayo na kuwapa nafasi watanzania kupata
bidhaa hizi katika viwanja hivyo zikiwa na bei nafuu kabisa.
Maonyesho hayo yametajwa kuwa ya
kipekee Tanzania hivyo amewahamasisha watanzania kuja na familia zao katika
maonyesho hayo ambapo amesema kuwa kutakuwa na vitu vingi sana ikiwemo michazo
ya watoto,na kadhalika hivyo watu wanahamasishwa kwenda kwa wingi
Aidha
NDAUKA amesema kuwa lengo la maonyesho hayo pia ni kukuza na kuendeleza
wafanyabiashara pamoja na kupanua zaidi masoko yao na kuwawezesha kufikia
malengo ya mafanikio huku akiwahakikishia watanzania usalama katika maonyesho
hayo
No comments:
Post a Comment