Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania kwa kupitia
kamati ya wanawake na chama cha mpira wa miguu kwa wanawake wanatambua umuhimu
wa siku ya wanawake duniani.Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo
inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani.Idadi ya
wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi
mwaka.
Katika
kusheherekea siku ya wanawake duniani
mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF
/TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa
miguu wanawake ni lazima kuanza na
vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa
mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.
Walimu
hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha
la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.
Ni
matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta
mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa
kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake
No comments:
Post a Comment