Saturday, March 8, 2014

REPORT MAALUM--KATIBA MPYA YALIGAWA KANISA KATOLIKI,SOMA HABARI24 ILICHOBAINI


 





Na Karoli Vinsent
  
         UJIO wa Katiba Mpya na Mjadala wa serikali ngapi zinafaa nchini ,sasa umeligawa kanisa Katoliki nchini habari24,imebaini.
          Habari za kuaminika ambazo mwandishi wa mtandao huu amezipata  na Kuthibitishwa na vyanzo mbalimbali ndani na nje kutoka kwenye Tume ya Haki na Amani ya Baraza la maaskofu wa Kanisa katoliki Tanzania(TEC) zinasema,

          Mgawanyiko huo umejionesha waziwazi baada ya Viongozi wakuu wa dini hiyo na Vyombo vyake,kuonyesha Dhahiri hawako pamoja kusimamia misimamo yao na kufanya waumini wao kubaki njia Panda.Habari24,imebaini.

            Hali hiyo imebainika mwanzoni mwa wiki  baada ya Tume ya Haki na Amani ya Barazala maaskofu wa Kanisa katoliki Tanzania(TEC).kutoa tamko ikitaka Bunge maalumu katiba kuepuka kukashifu kile walichokiita mapendekezo ya serikali tatu.

      Tamko hilo ambalo mwandishi wa mtandao huu ameliona ambapo katika  tamko hilo lilosainiwa na Mwenyekiti wa tume hiyo Askofu mkuu,Paulo Ruzuka amesema pendekezo la Serikali tatu litawarudusha watanzania katika hali ya kuwa wamoja na wenye kuaminiana.

       Tamko hilo lilizidi kufafanua kuwa muungano wa Serikali mbili haukutatua matatizo ya msingi na Badala yake ulilimbikizia kero zilizosababisha Zanzibar kujiundia katiba yake mwaka 2010 bila kushauriana na Tanzania Bara.

         Tamko hilo la kurasa 15 lilitolewa baada ya mkutano wa Kimataifa wa wajumbe wa kamati za majimbo za Haki na Amani za kanisa hilo na Chama cha wanataaluma wakatoliki Tanzania (CPT),uliofanyika Februali 5 mwaka huhu jijini Dar es Salaam.

         Msimamo wa Tume  ya Haki na Amani ya Barazala maaskofu wa Kanisa katoliki Tanzania(TEC). Unaonekana unapingana na ule uliotolewa mwanzoni  mwa wiki hii katika mkutano na Waandishi wa Habari na Askofu mkuu wa Kanisa katoliki Muadhama Policapy Kardinali Pengo ambapo alisema yeye ni muumini wa Serikali mbili.

         Pengo,katika mkutano huo alisema anamashaka  kuhusu  muundo wa Serikali tatu kwani hutokana na upendo,umoja na maslai ya wananchi wa Tanzania huku akipingana waziwazi  na TEC.

           Mtandao huu umebaini kauli aliyoitoa Askofu Pengo na
Tume  ya Haki na Amani ya Barazala maaskofu wa Kanisa katoliki Tanzania(TEC) umeonyesha wazi sasa kanisa hilo kubwa hapa nchini limeanza kulipasua kanisa hilo na kuwaacha waumini wake wakiwa njia panda wapi waende,kutokana na mikingano ya viongozi wao wa dini.

          Wachambuzi mbalimbali waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu wanasema mgongano huo unaojitokeza kwenye kanisa hilo ni wazi sasa watumishi wa kiroho wanaanza kujiingiza kwenye siasa huku wakiicha kazi yao kubwa ya imani,huku wengie wakisema kwanini Askofu pengo hawe tofauti na wenzake wa TEC wakati wao ni wamoja na mtengano huo unaweza kuonyesha sasa wazi  kuna watu wanatumiwa na wanasiasa katika kanisa hilo.

         Wachambuzi hao wakaenda mbali na kusema TEC basi wasingeutoa hilo tamko, kwani inaonekana limetolewa bila ya kuwashirikisha Maaskofu wenzake ,kama Wao wanasema serikali tatu inakuwaje Askofu Pengo mkubwa kama huyo anakuwa tofauti?au wakati wanapitisha hilo tamko walikuwa watu wachache na sio jumiya nzima ya TEC?

          Habari ambazo mwandishi wa Mtandao huu amezipata kutoka kwa waumini wa makanisa katoliki hapa nchini waliokuwa wazi kuzunguma na mwandishi wa mtandao huku wakitaka majina yao yasitajwe mtandaoni,walisema

         Wanashangaa kwanini viongozi wao wanakuwa wanatofautiana katika maamuzi,na kushangaa kwanini wanaingia kwenye siasa huku wakijua siasa ni vitu vya uongo kwani bibilia imekataa viongozi wa dini kuwa kwenye siasa,

         Ikumbukwe si mala ya kwanza kwa kanisa katoliki nchini kujiingaza kwenye masula ya kisiasa ikumbukwe kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 aliyekuwa Askofu msaidizi wa Jimbo katoliki la Dar es Salaam Methoid Kiraini aliibuka na kumnadi mgombea wa Urais wa mwaka huo_
 Jakaya Kikwete kwa kumuita Chaguo la Mungu,kauli hiyo iliwafanya waumini wa kanisa hilo pamoja na wanasiasa kuanza kuhoji kwanini viongozi hao wanajiingiza kwenye siasa,Tafakali

No comments: