Vurugu katika jamii hutokea kwa
wingi zaidi kuliko wizi
Lakini mara nyingi wananchi hawapati
msaada wa polisi wanaouhitaji
------------------------------
Karibu
nusu (46%) ya Watanzania wote wamearifu kuwa wameshawahi kushuhudia vurugu
katika jamii katika kipindi cha miezi sita iliyopita,ikilinganishwa na idadi ya
mtu 1 kati ya 5 (20%) anayeripoti kuwa amewahi kuibiwa kitu na wezi. Nusu (49%)
ya Watanzania wote wanaripoti kuwa hawajawahi kuibiwa kitu na watu 4 kati ya 10
(37%) hawajawahi kushuhudia vurugu/ghasia katika jamii.
Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika
muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, TukoSalama? Wananchi watoa taarifa
kuhusu hali ya usalama wa nchi. Muhtasari huu ni kwa mujibu wa takwimu
kutoka Sauti za Wananchi, utafiti kwa njia ya simu za mkononi wenye
uwakilishi
wa kitaifa uliofanyika kwenye kaya zote Tanzania Bara.
Wananchi wameripoti kuwa, kesi nyingi
walizoshawahi kusikia zinazohusu mtu kutishiwa, kupigwa mawe au kuuawa, huwa ni
makundi ya watu au watu binafsi wanaoyatenda na siyopolisi au jeshi.
Kwa mfano, mwananchi 1 kati ya 5 (19%)
ameshawahi kusikia habari za mtu kuuawa na kundi la watu, wakati ni wananchi 2
kati ya 50 (4%) tu walioshawahi kusikia mtukuuawa na polisi. Hata hivyo,wananchi
pia wamesema kuwa polisi mara nyingi huhusika
anapokutwa
mtu ametishwa, kupigwa au kupondwa mawe.
Wananchi wanapokumbana na uhalifu,
wangependa kuripoti polisi, ingawa, ni nusu tu yawananchi wote (47%) wanaofanya
hivyo. Idadi ni kubwa katika maeneo ya mijini ambako watu 6 kati ya 10 (59%)
waliripoti kuwa wangeweza kuripoti uhalifu polisi, ikilinganishwa na maeneo ya vijijini ambako watu 4 kati ya 10 (39%)
ndiyo wangefanya hivyo.
Hii inaweza kusababishwa na uwepo wa polisi kwenye maeneo ya mijini
kuliko vijijini. Kitaifa, kwa mujibu wa maafisa watendaji wa vijiji na
wenyekiti wa mitaa/vitongoji, jamii 6 kati ya 10 (62%) haina polisi.
Maeneo
ya mijini yana nafuu zaidi ambapo mitaa 4 kati ya 10 (36%) tu ndiyo yenye
ukosefu wapolisi, wakati maeneo ya vijijini takriban vijiji 8 kati ya 10 (76%)
waliripoti kutokuwa na maofisa wa polisi.
Walipoulizwa ni kwa nini watu hawaripoti
uhalifu kwa polisi, Watanzania wamelaumu rushwa au polisi kutowahudumia
ipasavyo wananchi. Mwananchi mmoja kati ya watano (22%)amesema kuwa atalazimika
kumlipa polisi kiasi cha pesa ili apatiwe msaada, na idadi kama hiyo ya
wananchi walisema kuwa polisi wasingewasikiliza au kuwajali wanapofikisha
taarifa kituoni.
Sauti za Wananchi pia
ilichunguza mtazamo wa watu kuhusu mfumo wa sheria. Kwa kawaida, watu
wanaporipoti uhalifu kwa polisi, ni haki yao kutarajia kuwa polisi watajaribu
kumkamatamhalifu na kisha kumfikisha mahakamani na hukumu kutolewa kwa mujibu wa
sheria. Kwa ujumla, Watanzania wana imani ndogo kama haya yanatendeka. Nusu yao
(52%) wanaaminikuwa kama mwananchi wa kawaida atafanya kosa/uhalifu,
hataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Jambo linalotia shaka, wananchi pia wana
mtazamo wa kuwa kuna kukosekana kwa usawa mbele ya sheria kulingana na hadhi ya
mtu: wananchi 7 kati ya 10 (67%) wanaamini kuwa mtutajiri hawezi kuadhibiwa kwa
uhalifu au kosa alilotenda, na wananchi 6 kati ya 10 wanaamini kuwa viongozi wa dini, maafisa wa polisi,
viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa umma hawawezi kuadhibiwa kwa
makosa/uhalifu wao.
Rakesh
Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Kutokuwepo kwa imani na mfumo wa sheria pamoja na utumiaji wa njia zisizo rasmi ili kupata haki kuna dhoofisha
usalama nchini. Upanuzi
wa mifumo rasmi ya usalama na kuipatia sekta ya
usalama rasilimali za kutosha ni sehemu ya
ufumbuzi wa tatizo hili, ila
bado hali inahitaji ubunifu zaidi na kufikiri kwa mapana. Masuala haya
yanahitaji mjadala mkubwa wa umma, ikiwa ni pamoja na kwenye michakato ya Bunge
la
Katiba."
No comments:
Post a Comment