Klabu ya Simba itafanya mkutano wa wanachama wake Jumapili
(Machi 16 mwaka huu) kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao.
Nachukua fursa hii kuwatakia kila la kheri katika mkutano
huo ambao ni muhimu katika kuhakikisha klabu yao inapiga hatua katika maendeleo
ya mpira wa miguu na ustawi wake kwa ujumla.
Hata hivyo, nawakumbusha viongozi na wanachama wa klabu ya
Simba kuwa marekebisho hayo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia Katiba, Kanuni
na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika (CAF)
na Tanzania (TFF).
Aidha waraka wa TFF kwa wanachama wake wa Februari 7 mwaka
huu uzingatiwe kikamilifu katika marekebisho hayo.
TFF inawatakia wanachama wa Simba mkutano mwema, na
inawakumbusha wazingatie umuhimu wa kudumisha amani na maelewano katika klabu
yao.
No comments:
Post a Comment