Mkuu wa mkoa wa Dar es Saalam akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema hii leo. |
Kile kinachoonekana kama liwalo na liwe,
leo hii mkuu wa mkoa wa Dar es Salam ametangaza rasmi kuwa serikali yake
haitawajibika kwa matatizo yoyote yatakayojitokeza kwa wale wananchi
wanaokaa mabondeni, na zile sehemu hatarishi ambazo uwezekano wa kukubwa
na mafuriko ni mkubwa na kwamba yeyeote atakayengoja mafuriko yamkute
ndipo aanze kulaumu serikali,hiyo itakuwa ni kazi ure,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salam, Mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua imekkuja kufuati wakazi wa maeneo hayo kukaidikuondoka kwa hiari na hata serikali ilipotaka kuwaondoa kinguvu bado wamekuwa wakaidi na kuamua kufngua kesi mahakamani wakiitaka mahaka kuweka hati ya zuio ili wasieze kufukuzwa katika maeneo yao,
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini, mkuu wa mkoa wa Daresalaam akifafanua jambo mbele yao. |
Sadiki ameongeza kusema kuwa sasa hakuna
msalie mtume, Tatizo lolote litakalojitokeza katika mabonde hayo watajua
wenyee wapeleke wapi vilio vyao kwani sasa serikali imenawa mikono
kuhusiana na kadhia hiyo
Ameongeza kusema kuwa, wananchi wafahamu
kuwa serikali haina nia ya kuingilia muhimili mwingine wa serikali kwa
kuwafukuza maeneo yao yanayokaa, lakini wafahamu kuwa serikali haitakuwa
pamoja kwa madhala yoyote yatakayojitokeza.
Kama
unavyojua Tayari mamlaka ya hali ya hewa imeshatoa angalizo kuhusiana
na mvua zinazoendelea jiji Dresalaam , hivyo watu wa mabondeni ni vyema
wakatoka wenyewe kuliko kungoja mpaka mafuriko yawafunike ndipo
unakumbuka kuhama, na huko hakuna na tofauti na kukumbuka shuka wakati
kumeshakucha
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa
mkoa wa Daresalaam amewataka wakazi wa Daresalaam kuhudhlia katika
sherehe za siku ya mwanamke ambayo itafanyika march 8 pale mwembe yanga,
huku mgeni rasmi akiwa waziri wa jinsia na watoto.
Meck Sadick amesema kuhudhulia kwa
wananchi ndio kufankisha kwa sherehe hizo, hivyo i vyema wakatumia muda
wao kuja kusherehekea kwa pamoja siku ya mwanamke ambayo kwa mwaka uu
inakaul mbiu nzuri inayochochea kuheshmiwa kwa haki za mwanamke hapa
nchini
No comments:
Post a Comment