Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Umoja wa
Katiba ya Wananchi UKAWA,kususia vikao vya bunge maalum la Katiba kutokana na uonevu kutoka kwa wajumbe wa Chama
cha Mapinduzi CCM.
Hivi, leo nao umoja wa Asasi za Kiraia AZAKI umeibuka na kumtaka Rais Jakaya Kikwete
kuvunja Bunge la katiba
maramoja,kutokana na wajumbe hao kuanza kujadili katiba yenye maslai yao na
kusahau wananchi ambao ndio waliowatuma.
Hayo,yalisemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mweyekiti wa umoja wa umoja wa asasi za Kiraia AZAKI, Irenei Kiria wakati wa mkutano na Waandishi,ambapo
alisema hawajafurahishwa na mijadala ndani ya Bunge la Katiba,
“Sisi umoja wa Asasi za Kiraia
hatujaridhishwa na mijadala ndani ya Bunge Maalum la kutunga Katiba,mijadala
ambayo imepoteza Utaifa na badala yeke kujikita kwenye
kutoheshimiana,ubabe,ubaguzi,vijembe na Vitisho kutoka kwa wajumbe”
“Tunaona kwamba Mwendendo wa
Mijadala ni kuelekea kuteta maslahi ya watawala na vyama vya siasa badala ya
maslai ya utaifa na ustawi wa wananchi”Alisema Kiria
Kiria,alizidi kusema wao
hawajalizishwa na maauzi ya wajumbe hao wa bunge hilo kupendekeza kufuta vitu
muhimu kwenye Katiba.
“kwamba kitendo cha Baadhi ya
Wajumbe kupendekeza kutoa maneno,uwajibikaji,uadilifu,uwazi katika kipengele
cha tunu za Taifa inatia shaka kama nia ya Bunge Maalumu la katiba na kutuletea
katiba itakayotatulia matatizo yao”
“Vilevile pia hatujafurahishwa na
kufungiwa Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.Na hakuna juhudu zaSerikali
kuwafikishia wananchi Rasimu ya pili ya Katiba,kwahiyo sisi tunaona kwa Rais
Jakaya Kiwete avunje Bunge hili la Katiba”aliongeza Kiria.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kituo
cha Sheria na Haki za binadamu Bi Kijo Bisimba naye alisema Rais Jakaya kiwete
amepwaya katika kusimamia mchakato huo wa Katiba kutokana na Kitendo chake cha
kufuata matakwa ya Chama chake.
“Kiukweli Rais Kikwete wakati ananza
mchakato huu hadi kuunda Tume ya kukusanya maoni alianza vizuri,Lakini
amekuja kuchemsha baada ya kutoa hutuba yake wakati akifungua bunge Maalum la
katiba ameonekana wazi kabisa anaanza kufuata matakwa ya chama chake,na yeye
ndio alianza kuharibu mchakato wote wa katiba”alisema Bisimba.
Naye,Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba
Deus Kibamba,ambaye taasisi yake ndio inayounda AZAKI,alisema Rais Kiwete avunje
bunge hilo la Katiba kutokana na Mambo yanayoendelea katika bunge hilo.
“Kiukweli wote mashahidi akuna
kinachofanyika mule Bungeni zaidi ya vijembe tu na kila mtu akitetea
maslai ya chama chakee na kuwasahau wananchi,na Hata Kauli aliyoitoa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi ni wazi
hakuna kinachojadilwa bungeni,na kama rais Kikwete anamapenzi mema na nchi yake
na kujenga heshima basi avunje bunge hilo la katiba haraka sana”alisema Kibamba
Haatua hii ya AZAKI imekuja siku
moja tu kupita baada ya umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kususia bunge hilo la
katiba kwa kile wananchodai ni ufedheheshaji na kuwagawa wananchi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa
Bunge) kutokana na Kauli zake.
Hatua ya kususia vikao hivyo
ilitolewa na Profesa Lipumba jana bungeni ambapo alianza kwa kunukuu Gazeti la
Mwananchi la Aprili 14, mwaka huu katika sehemu inayosema;
“Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) ameanza kampeni kanisani kwa kuwataka
wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa serikali ya muungano
itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.”
Alisema yeye ni muumini wa dini ya
Mwenyezi Mungu lakini anaafiki mapendekezo yaliyoletwa bungeni hapo na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba iliyoundwa na Rais.
“Hii ni kauli ya Waziri Lukuvi ndani
ya Kanisa la Methodist wakati wa sherehe ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala
kuwa Askofu na Waziri Lukuvi alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu.”
Alisema inasikitisha kwa sababu
kauli hiyo inafanana na ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akihutubia
Bunge Maalumu.
Alisema kauli za Lukuvi zinatisha
baada ya kusema Wazanzibari ambao wanataka kuwa na nchi yao hawawezi
kujitegemea, bali wanataka wapate nafasi ya kujitangazia kuwa ni nchi ya
Kiislamu.
“Waziri anaweza kusema hivyo ndani
ya kanisa? Kawahamasisha mpaka yule kiongozi wa kanisa akasema ili kudumisha Muungano
bora Katiba ya Zanzibar ifutwe ili iwepo moja ya nchi moja ambayo inadumisha
Muungano,” alisema.
“Kama ndugu zetu wa Zanzibar
wangekuwa wanahitaji serikali moja tungekuwa na utaratibu mzuri tu, lakini siyo
wanachama wa CUF, siyo wa CCM, Wazanzibari wote hawataki muungano wa serikali
moja,” alisema.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba
imetoa mapendekezo ya serikali tatu kutokana na ukweli huo. “Hoja zilizoletwa
hapa ni hoja za serikali moja, si hoja za serikali mbili lakini wenzetu moja
hawataki, kwa hiyo tunahitaji Muungano ambao tutakuwa na maridhiano ya pande
zote mbili,”
No comments:
Post a Comment