
Rais
Jakaya Kikwete, amesema kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu, kwa
baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi wa Taifa
la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume.
Rais
Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi
makubwa na ya kihistoria, kiasi cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha
na kuenzi heshima yao kwa namna ya kudumu.
Rais
Kikwete ametoa msimamo huo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu matusi, kejeli,
dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa Bunge Maalum la
Katiba juu ya waasisi hao wa Tanzania na Wabunifu Wakuu wa Muungano wa
Tanzania.
HABARI HII NI KWA MSAADA WA https://www.facebook.com/eatv.tv?
No comments:
Post a Comment