Kamishna wa polisi kanda maalum ya dar es salaam SULEMAN KOVA akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam |
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum D’Salaam linawashikilia watuhumiwa 13 ambao wanahusishwa
na tukio la ujambazi lililotokea tarehe 15/4/2014 majira ya saa tatu na nusu
asubuhi katika Tawi la Benki hiyo Kinondoni.
Watu
wenye silaha aina ya SMG na Bastola waliingia ndani ya benki ya Baclays na
kupora kiasi cha pesa T.Shs.390,220,000, USD 55000, UERO 2150 na Pound 50.
Majambazi waliwatishia kwa silaha watumishi wa
benki hiyo na kuwaweka chini ya ulinzi na hatimaye kutoroka na pesa hizo kwa
kutumia pikipiki aina ya Fekon.
Awali majambazi hayo yalifika katika benki
hiyo wakiwa na magari 2, gari moja aina ya OPA lenye namba T.421 BQV rangi ya
Silver ambayo sasa imekamatwa.
Wanahabari mbalimbali wakiwa kazini katika mkutano huo wa kamishna kova na wanahabari leo jijini dar es salaam |
Majambazi
hao walianza kusakwa na vikosi mbali mbali vya Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja
na Kikosi Maalum (Task Force) ambacho ni Maalum kwa kuzuia na kupambana na wizi
katika mabenki jijini D’Salaam. Kati ya
watu waliokamatwa ni pamoja na Meneja wa benki katika Tawi hilo
1. ALUNE D/O KASILILIKA @ MOLLEL, MIAKA 28,
MKAZI WA KIMARA BONYOKWA, ambaye uchunguzi wa kina unaonyesha kwamba Meneja
huyu alishirikiana na mfanyakazi mwenzake ambaye ni Meneja Operesheni wa benki
hiyo aitwaye 2. NEEMA D/O BANDARI @ BACHU kwa kula njama na watu wengine na
majambazi ambao kwa pamoja walifanikisha tukio hilo la wizi wa fedha katika
tawi hilo. Aidha katika tukio hilo imegundulika
kwamba robo tatu ya fedha zote zilizoibiwa zilichukuliwa kabla ya siku ya tukio
la ujambazi tarehe 15/4/2014.
3. FREDRICK S/O LAZARO miaka 19, mkazi wa
Manzese
4. KAKAMIYE S/O JULIUS miaka 31, mkazi wa
Kinondoni
5. IDDI S/O NGUVU @ HAMISI miaka 32, mkazi wa
Kinondoni
6. SEZARY S/O OSWARD MASAWE @ MSOLOPA
7. BONIFACE S/O NDARO @ MUUMBA miaka 29 mkazi
wa Kijitonyama
8. ERASMUS
S/O BERNARD MROTO @ MENYEE miaka 38 mkazi wa Magomeni
9. DEO S/O ISDORI OLOMY miaka 32, mkazi wa
Manzese Darajani
10. MOHAMED
S/O ATHUMANI @ SALUM miaka 31, mkazi wa Kimara Stopover
11. JOSEPH S/O MKOI miaka 33, mkazi wa Kimara
Stopover
12. LUCY D/O AMOS @ MACHA miaka 30, mkazi wa Tabata
13. GRACE
D/O AMON @ MACHA miaka 39, mkazi wa Kibaha
Aidha
baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wamehojiwa na kukiri kuhusika na wizi huo na
walipopekuliwa walipatikana na fedha kiasi kidogo ambazo ni sehemu ya mgao
waliopata baada ya tukio hilo. Vile vile kabla ya tukio imebainika kuwa
kulikuwa na vikao mbali mbali vya maandalizi ya kufanikisha tukio hili kabla ya
tarehe 15/4/2014 ambayo ni siku ya tukio.
Upelelezi
wa shauri hili bado unaendelea, tunaomba wananchi/raia wema waendelee
kusaidiana na Jeshi la Polisi kwa kutupatia taarifa ili tuweze kuwakamata wote
waliohusika na tukio hilo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment