Na Karoli Vinsent
MBUNGE Wa Tabora Mjini,Ismahil Aden
Rage ametoboa Siri ya Kufanya Vibaya kwa Chama cha Demokrasia na Maendereo
CHADEMA katika Chaguzi mbalimbali hapa nchini,na kusema chama hicho
kingojee Miujiza ili Kiweze Kushika Dola.
Rage,aliyasema leo Jijini Dar es
Salaam,alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu na kusema kwa sasa Chama
hicho kimepoteza mvuto kutokana na kuendeleza Siasa za Majitaka na kujuana
kutoka kwa Viongozi wajuu wa Chama hicho,kutokana na kitendo cha chama hicho
kumvua Uongozi na Uanachama Naibu Katibu Mkuu Bara Zitto Kabwe.
“Kiukweli acha niseme Ukweli,Chadema
kimepoteza Mvuto sana hususani kwa Vijana kutokana na Kitendo chake cha
kumuondoa Zitto Kabwe,na ukweli ni kwamba huyu mtu anapendwa sana na Vijana
sana mpaka ikafikia hatua hata sisi viongozi wa Chama Tawala tulikuwa tunapata
Tabu sana,”
“Leo Mwenyewe ni shuhuda Baada ya
chama hicho kumvua Zitto Kabwe, uongozi pamoja na Uanachama tayari CCM,imeanza
kupata ushindi kwenye Majimbo mbalimbali.Na hata mvuto wa chama hicho kwa
Wananchi umeanza kupotea kuliko mwananzo,”alisema Rage.
Rage,ambae pia ni Mjumbe wa Maalum
la Katiba,katika hatua nyingine aliwataka Wajumbe wenzake wa Bunge la katiba
kutoka UKAWA.warudi ili waendelee kutengeneza katiba ya Wananchi,kwani kufanya
hivyo akukubaliki na Muungwana hana Budi kusamehe.
Rage,vilevile ni Mwenyekiti wa Klabu
ya Mpira wa Miguu ya Simba,alizidi kuongeza kwamba Rais Kikwete amefanya Jambo
jema sana kuanzisha mchakato huu wa kupata katiba mpya,kitendo cha UKAWA
kufanya hivyo kutaifanya mchakato huo wa katiba kutofanikiwa na kupelekea pesa
za walipa kodi kupotea kodi bule
No comments:
Post a Comment