"Mwigulu Nchemba anataka Serikali moja, lakini
anaogopa kusema"........... "Mhe.Mwenyekiti, kwanza naunga mkono
Serikali tatu kama zilivyoletwa kwetu na TUME ya Katiba ya Jaji Warioba, kwa
hiyo tunaunga mkono maoni Wananchi. Aliyeuharibu huu mchakato ni RAIS aliyekuja
kueleza msimamo wa Chama chake badala ya kuzindua Bunge. Hiki ni Kipindi cha
Kwaresma, acheni unafiki, tumeharibu Pesa nyingi.
CCM wameishiwa hoja,
wameanzisha mkakati wa kuzomea. MWIGU...LU anataka Serikali moja, lakini anaogopa kusema. Tupo
kwenye nafasi nzuri sana ya kulijadili Swala hili, la sivyo, tutalijadili kwa
kulazimishwa. Leo LUKUVI anatutishia uwepo wa Serikali tatu, JESHI litaitawala
Nchi! Mbona Rais wetu alikuwa Mwanajeshi na anatuongoza?...Wanajeshi ni Ndugu
zetu, wakitawala kuna tatizo gani?...
Unapopimwa Malaria au Ukimwi, Sample ya
Damu inatolewa kidoleni, na sio lita tano ili kujua ngoma imekaaje mwilini!
acheni kutuzingua kwamba waliohojiwa na TUME ya Warioba ni wachache". amesema
Mhe.Sugu.
No comments:
Post a Comment