Wednesday, April 9, 2014

EXCLUSIVE---SOMA ALICHOKISEMA TUNDU LISSU BAADA YA SPIKA SITTA KUMWOMBA RAISI AONGEZE MUDA WA BUNGE MAALUM



Na Karoli Vinsent

          SIKU moja kupita Tangu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Samweli Sitta kumuangukia Rais Jakaya Kikwete kumuomba aongeze  Muda,Naye  Mwanasheria wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Tundu Lissu amevaa na kumwambia Wao hawatakubali siku 20 kuongezwa na watapinga kwa nguvu kama Rais atafikia maamuzi ya kuziongezwa.

        Hayo,yamesemwa Leo na Tundu Lissu wakati wa mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu  kuhusu ombi la Mwenyekti wa bunge Maalum la katiba Samweli Sitta kwa Rais Kikwete kuongeza mda wa Siku 20.ambapo alisema wao hawatakubali siku kuongezwa kwasababu Bunge halijadili kifungu chochote.
         
      “Mpaka sasa hivi hatujajadili kwenye bunge Maalum ibara hata moja,katika  ibara 271 za Rasimu hatujajadili hata moja na kufanyia uamuzi sasa hizo siku 20 alizomba kuongezwa ni za nini kama sio Ujinga anataka kufanya?”alihoji Lissu.
      
          Tundu Lissu,ambaye pia ni Mwanasheri wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alizidi kusema kwanini Sitta anaenda kuomba muda kuongeza wakati mda huu wa Siku 70 bado ujaisha.
         
         “Sheria inasema kama muda wa Siku 70 hautoshi Mwenyekiti wa Bunge la Maalum  atashauriana na Rais pamoja na Rais wa Zanzibar kuhusu muda gani unafaa,sasa leo ukiongeza siku 20 hatuta fanya kazi yeyote na kama yeye Sitta anakimbilia kuomba kuongeza wakati sisi hapa hatujaanza kazi yeyote”

     “kwahiyo yeye asema ukweli kuhusu kuomba kuongeza siku 20 ni kutafuta namna na kuhujumu  mchakato huu wa katiba sisi hatutakubali kwani ni njama za kuvurugha na kuhujumu mchakato wa Katiba  Mpya”alisema Lissu.
        
           Lissu ambaye vilevile ni Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA alisema kwa sasa wao wanangojea tamko Rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa bunge hilo la katiba ili wachukue hatua ya kugomea hatua hiyo.  

No comments: