Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani
Afrika kwa mwaka 2013 Heshima
hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African
Leadership Magazine Group na Tuzo hiyo ya heshima itatolewa leo jioni katika
sherehe iliyopangwa kufanyika mjini Washington, D.C, Marekani
Tuzo
hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ambaye tayari amewasili mjini
Washington kuhudhuria sherehe hiyo
Tuzo
hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango
mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa wananchi
No comments:
Post a Comment