Na Karoli Vinsent
BAADA ya Mwandishi wa Gazeti la Sunday Mail la
Nchini uingereza Martini Fletcher kuandika makala nyingine ikihishutumu
tena serikali ya Jakaya kikwete kwa kushindwa kuwachukilia hatua Majangili.Hivi
leo waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Piter Msigwa amewamvaa watu
waliokuwa wakimbeza mwandishi huyo,na kusema walikuwa hawataki kuambiwa ukweli
juu ya ujangili unaofanywa ndani ya nchi.
Mchungaji Msigwa aliyasema hayo Leo
wakati wa Mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu,ambapo alisema alichokifanya
mwandishi ni sahihi kwani alichokiandika mda hule watu wengi walimbeza yeye
“Leo mmejionea wenyewe baada ya kuandika
makala nyengine amezidi kusema ukweli juu ya Serikali ya Rais Kikwete kwa
kushindwa kupambana na vitengo vya ujangili juu ya Tembo,na katika makala ya
kwanza mlikuwa mnanilaumu mimi kuwa sina uzalendo kutokana na mimi kumwambia ukweli,
wakati kuna haja ya kusema ukweli juu ya biashara hii haramu”alisema Msigwa
Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa
Mjini kupitia Chama cha Demokrasia maendereo CHADEMA alizidi kusema serikali ya
Rais kikwete bado imeshindwa kupambana na vitendo vya Ujangili nchini na
mwandishi huyo amesema hivo hivo.
“Mwandishi huyo amekuja tena mara ya
pili, licha ya serikali kutumia Garama kubwa kumlipia Usafiri wa Ndege,garama
za Hoteli pamoja na kumtembezwa kwenye pori la akiba Selous na Hifadhi ya
Serengeti”
“Ili akaisafishe serikali kwenye
medani za kimataifa ,lakini bado ameenda kuandika ukweli juu ya udhaifu wa
serikali katika vita vya ujangili hapa nchini,kwa upande wangu nampongeza sana
Martini Fletcher kwa ushujaa wake nawaomba waandishi wa Tanzania waige mfano
huu waache kuwa walamba viatu vya Tabaka tawala kama hili lenye maovu mengi”
alisema Msigwa.
Makala yake aliyoitoa Februali 8
mwaka huu na kuchapishwa kwenye Gazeti la Sunday Mail ambapo katika makala hiyo
alimtuhumu Rais kikwete kwa kushindwa kuwachukulia hatua vinara wa vitendo vya
ujangili
Vilevile, Makala hiyo ikizidi
kumtuhumu Kikwete kwa kumdharau aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii Barozi
Khamisi Kagasheki alipokuwa anamletea Orodha ya vinara wa vitendo vya ujangili.
Baada ya kuandika Makala hiyo
Rais Kikwete wakati alipokuwa nchini uingereza anahojiwa kwenye kituo cha
televishieni cha CCN alikanusha taarifa hiyo na kusema serikali yake imefanya
kazi kubwa ya kukomesha vitendo vya ujangili hapa nchini.
Serikali ya Tanzania kwa kile
kinachotafsiriwa ni kujikosha kwa Mwandishi huyo,walimwita na yeye aliwasili
nchini wiki tatu zilizopita na kufikia kwenye hoteli ya Kimataifa ya Serena na
Baadae kutembelea pori la akiba Selous na Hifadhi ya Serengeti.
na vilevile inasemekana
alionana na Rais wa Jakaya kikwete ili Mwandishi huyo abadili kile
alichokiandika kwenye makala yake.
Makala ya Fltecher kwenye Gazeti
hilo la Uingereza,yaliwakasirisha viongozi wa Tanzania hususan Rais Kikwete
hasa kutokana na ujio wake ulilenga muda ambao viongozi wa mataifa zaidi ya 50
walikuwa wamealikwa kwenye mkutano maalum ulioitishwa na mwana wa Mfalme wa
Uingereza,Prince Charles,mjini London.
Lakini Mwandishi akazidi kuonyesha
umakini wake katika fani yake ya uandishi wa Habari na kuzidi kuivua nguo tena serikali ya Kikwete
na kumuumbua,kwani alitoa makala nyingine inayoonyesha udhaifu wa Serikali ya
Rais Kikwete kwakushindwa kusimamia ujangili nchini.
Katika Makala yake hiyo ya Jumapili
ya Tarehe 23 mwezi huu alimshutumu Rais Kikwete kwa kushindwa kuwachukulia
Hatua Majangili huku akiwajua kabisa wanapokaa.
Makala hiyo ilizidi kusema Chama cha
Mapinduzi CCM ambacho ni Chama anachotoka Rais Kikwete ndio vinara wa Vitendo
vya ujangili, ,vilevile Ndio sababu Rais kikwete kushindwa kuwachukulia hatua
Majangili.
No comments:
Post a Comment