habari kwa hisani ya selemani Magari fullhabari blog
Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya
ufundi Mh. Jenista mhagama, amewataka maafisa elimu, wakurugenzi wa
elimu na wakuu wa Chuo kuwapokea kwa mikono miwili walimu wapya
walipangiwa katika halmashauri zetu ili walimu hao wajione kama wamefika
katika mikono iliyo salama katika kazi zao,
Akizungumza katika uzinduzi wa vitabu
vya uchambuzi wa matokeo kwa kidato cha nne ya mwaka 2013, Mhagama
amesema, serikali imewapangia jumla ya walimu 18093 katika halmashauri
mbalimbali hapa nchini ambao kati yao walimu wa stashada ni 5416 na wale
wa shahada ni 12677 wanaotarajiwa kuripoti kwa wakurugenzi kuanzia leo
ili wapangiwe vituo za kufanyia kazi,
Mhagama amesema walimu hao wanatarajiwa
kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walimu unaolikuta taifa kwa shule
zetu za kata na hata zile za misingi ambazo kwa mda mrefu kumeonekana
uhaba wa walimu hao,
Wadau wakimsikiliza kwa makini naibu waziri alivyokuwa akiwataka kuwapokea kwa wema walimu wapya |
Amesema katika kuhakikisha Taifa
linaboresha mfumo wake wa elimu kwa kuongeza ufanisi katika sekta hii,
serikali imejipanga vizuri kuhakikisha walimu wanaoingia katika fani hii
hawajutii uwepo wao, na kwa kuanzia tunawaomba maafisa elimu kutusaidia
kwa kuwapokea walimu hao kwa mikono miwili ili wajione hawakukosea
kusoma fani ya ualimu
Katika uzinduzi huo wa vitabu vya
uchambuzi, Mhagama, alifanikiwa kugawa baadhi ya kopi za vitabu hivyo
kwa Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu(ELIMU) Mh. Kassimu
Majariwa
Naibu katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Bi Consolata Mgimba hapa nchini akifafanua baadhi ya mambo, |
No comments:
Post a Comment