KAULI ya wahenga inayosema “Mdomo
ulimponza kichwa”sasa ndiyo yanamkuta sasa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi,
Baada ya leo Jumuiya ya Uamsho na
Mihadhara ya Kiislam kuibuka na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumfukuza Kazi
Waziri Lukuvu,na kama Akikaida basi,Umoja huo hautamburuza Mahakamani.
Kauli,hiyo kali imetolewa Jijini Dar
es Salaam,na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam ,Abdallah
Said Alli,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema
wamesikitishwa sana na Kauli za Kichochezi na kuligawa Kidini Taifa,na
kupakizia sifa mbaya umoja huo.
“Sisi tumesikitishwa sana na Kauli
aliyoitoa Waziri mkubwa kama Yule,aliyoitoa Kanisani na Baadae akaja kuitoa
Kwenye Vikao vya Bunge la Katiba,eti akitushutumu sisi kwamba ndio tunahusika
na vitendo Viovu,na vilevile kutuhusisha na Chama cha Wananchi CUF”
“Mpaka Hivi sasa Hakuna Ushahidi
wowote uliowahi,kutolewa na Kuthibitishwa na kuihusisha UAMSHO na Vurugu
zozote zilizowahi, kutokea pale Zanzibar”alisema Alli
Vilevile,Katibu huyo alisema kwa sasa
wameamua Kumwandikia Mwenyekiti wa Bunge Maalum La Katiba Samweli Sitta.
“Tumemwandikia Barua Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samweli Sitta ili
atuambie ukweli kauli aliyoitoa Waziri Lukuvi,inahulali au la na tumemwambia
ukweli sisi hatuhusiki na upande wowote wa Chama cha Kisiasa”
“Kwasabu Jumuiya Hii imesajiliwa kihali
kabisa na Serikili ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya shuguli za kutoa elimu ya
Dini ya Kiislam, sasa inakuwaje waziri mkubwa,kama huyu anaongea Habari za
Kichoche Serikali inamwangalia”
Aidha Katibu huyo alisema kwa sasa
Wanamuomba Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi au amwajibishe Waziri Lukuvi.na
kama Rais akipuuzia Basi umoja huo utamfikisha Mahakamani ili akathibitishe
kile alichoongea pale Bungeni.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Elimu na
Habari wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam ,Saidi Amour
Salim,alisema Waziri Lukuvi ni mtu wa kupigwa vita na asiyetakiwa popote kwa
Vitendo vyake vya kuligawa Taifa na kupeleka nchi kwenye machafuko.
“Serikili naishangaa kwanini wanamfumbia macho waziri huyo wakati
anatugawa taifa.tena ndugu zangu anasema UAMSHO ni taasisi ya Kisiasa,wakati
sio kweli tena nataka kumwakikishia Lukuvi,Baada ya Rais Kikwete kufanya
Mabadailiko Jeshi la Polisi Zanzibar na kumteua Kamanda, nay eye ametuita kwa
Amani na kutuomba tukatafute njia ya kufanya Kazi kwa Amani”alisema Salim
Kauli hiyo inayodaiwa na Jumuiya hiyo
ilitolewa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi,Bungeni jijini Dodoma wakati alipotakiwa kutoa ufafuzi juu ya kauli zake
alizozitoa kanisani.
Ambapo,lukuvi Mambo mengi
wanayoyasema wanachama wa CUF ndiyo yanayosemwa na taasisi hiyo, hivyo kwa hofu
yangu binafsi, sina shaka Uamsho ni CUF kwani hata Wazanzibar wenyewe wanajua
hilo,’’ alisema.
‘’ Hatujawahi kuona Chama kinachojitayarisha kuchukua madaraka kinatumia
mgongo wa dini kufanya siasa. Hii si sahihi, kwanini nisiwe na hofu na
kusema,’’ alisisitiza
Akizungumzia Jeshi kuchukua madaraka,
Lukuvi alisema hofu yake hiyo imetokana na rasimu ya katiba, ambayo
inapendekeza kuwepo kwa serikali tatu, jambo ambalo serikali moja ya Muungano
vyanzo vyake vya mapato havikuwekwa wazi.
“Haya
yalikuwa ni mawazo yangu binafsi na sikuwa na shida kuyaeleza na nitaendelea
kuyaeleza na kisiwe chanzo cha wanachama wa UKAWA kudai kuwa hiyo ni lugha ya
uchochezi.
“Hivi kati ya mimi na Maalim Seif
(Katibu Mkuu wa CUF) nani ni mchochezi ? Mbona hawakugomea kauli yake aliyoitoa
Kibanda Maiti kuwa Rais Kikwete atamtuma Mkuu wa Majeshi Mwamunyange kwenda
kupindua nchi iwapo serikali tatu zitapita,’’ alisema lukuvi.
No comments:
Post a Comment