Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya tigo
leo imetangaza rasmi kuingia katika Ushirikiano mkubwa na kampuni maaarufu ya FACEBOOK
ambapo wateja wake wote wataweza kupata huduma za facebook kwa lugha ya
kiingereza na kwa mara ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao za
mkononi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mtandao wa Tigo DIEGO
GUTIEREZ amesema kuwa hii ni kwa mara ya
kwanza kwa mtandao wa facebook kupatikana bila malipo katika eneo hili la Africa
mashariki.
Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo
mkurugenzi huyo wa tigo amesema kuwa hii inamaanisha kwamba wateja wa tigo kwa
mara ya kwanza watakuwa na uwezo wa kutumia facebook kupitia simu zao za
mikononi bila kukatwa gharama za aina yoyote hivyo kuwawezesha kuungana na
wateja zaidi ya million mbili wa wanaotumia mtandao huo hapa nchini Tanzania.
Amesema kuwa hii pia ni kwa mara ya kwanza kwa mtandao wa kijamii kama facebook kupatikana kwa lugha ya kuswahili lugha ambayo inayotumika na watanzania wote ambapo amesema kuwa ni njia nzuri ya kuitangaza lugha hiyo kimataifa zaidi.
Naye mkurugenzi wa FACEBOOK wa ushirikiano na ukuaji
wa kimataifa NICOLA DE ELIA amesema kuwa wanayo furaha kubwa sana kwa
kushirikiana na tigo kwa mara nyingine tena na kuwapatia watanzania wengi zaidi
uwezo wa kuwasiliana kupitia utumiaji wa bure wa data katika app ya facebook na
tovuti ya simu na sasa katika lugha ya kuswahili.
Mkakati huu ni muendelezo wa mpango wa facebook
unaoitwa internet.org uliozinduliwa na muasisi wa mtandao huo MARK ZUCKERBERG
No comments:
Post a Comment