Creativr Base Company ltd
kupitia Kurugenzi yake ya Sanaa na Burudani kwa ujumla imeandaa kongamano la
kitaifa (National Film Summit 2014, NFS
2014)ambalo litafanyika mwezi June 2014 hapa Dar es Salaam katika ukumbi wa
Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)jengo la Mawasiliano Tower, Ubungo.
Lengo la kongamano hilo ni
kuunga mkono juhudi za Serikali kuitambua tasnia za filamu, kujadili changamoto
zilizopo katika mfumo mpya wa uwekaji wa stamp za kodi katika kazi za fIlamu na
muziki na namna ya kukabiliana nazo, kujadili changamoto za uzalishaji wa kazi
bora za filamu na masoko yake,Hakimiliki na hakishiriki za kazi za Wasanii
pamoja na umuhimu wa sera na sheria mbalimbali katika kusimamia tasnia ya
Filamu Tanzania kwa Maslahi ya Taifa na kukuza pato la Wasanii nchini, Kutafuta
ufumbuzi wa kudumu katika kuondoa tatizo la wizi wa kazi za Wasanii
Tanzania,kuanzishwa mawanda ya ushirikiano na Wasanii wengine wan chi za Africa
Mashariki na Kati.
Kutokana na
umuhimu wa tasnia ya filamu Tanzania, kamati ya Maandalizi ya .N.F.S ilikuwa na
mchakato wa kutafuta balozi wa N.F.S 2014, kutokana na mchakato huo jumla ya
Majina kumi na mbili ya Wasanii na waongozaji wa filamu Tanzania yalipendekezwa
kuingia katika uteuzi wa Balozi wa National Film Summit 2014.
Kutokana majina hayo kamati ya
maandalizi ya N.F.S 2014 imemteua Ndugu Emanuel Myamba (Mkurugenzi wa Chuo cha
Filamu Tanzania cha TFTC) kuwa Balozi wa National
Film Summit 2014 – 2015.
Mtaweza kujiuliza kwa nini kamati
imemteua Emanuel Myamba kuwa Balozi wa National Film Summit 2014, Wasanii
waliopendekezwa wana viwango sawa katika kazi zao lakini kuna cha ziada
amabacho Balozi anatakiewa kuwa nacho ili kuonesha tofauti na washindani
wengine,Kamati imemteua Emanuel Myamba kwa sababu pamoja na kuwa msanii mwenye
mafanikio katika kazi za uongozaji na uchezaji wa filamu pia ameweza kuwa na
kuwa na kituo mafunzo yakozi za tasnia ya filamu jambo ambalo ni muhimu kwa
maendeleo ya Wasanii kuwa na Elimu, hivyo amewewezakuisaidia Serikali katika
kukuiZa weledi wa Wasanii wachanga walio wakongwe kielimu.
No comments:
Post a Comment