Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono
wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na
kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.
Sehemu ya wageni
waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo
zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kikosi cha
Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
Kikosi cha Wanamaji
Ndege za kivita
zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye
Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
Maandamano ya Pikipiki.
Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50
No comments:
Post a Comment